MAHAKAMA
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman
Mbowe ya kutaka asikamatwe hadi kesi yake ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda itakapomalizika.
Maombi hayo
yalitupwa kwa sababu kifungu cha sheria kilichotumika kuyafungua si
sahihi na kwamba hutumika pale ambapo sheria ziko kimya.
Uamuzi
huo wa majaji umefikiwa kutokana na pingamizi la jamhuri
lililowasilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu Gabriel Malata kuiomba
kuyatupilia mbali maombi hayo kwani hayana msingi kisheria.
Katika
hatua nyingine, mwanahabari nguli nchini Jenerali Ulimwengu, ameungana
na jopo la mawakili Tundu Lissu, Peter Kibatala na John Malya katika
kumtetea Mbowe.
Mbowe amefungua kesi hiyo ya kikatiba namba 1, ya
mwaka 2017 dhidi ya wadaiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na
Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Kesi
hiyo itasikilizwa tena Machi 8, mwaka huu.
Maombi hayo
yalitupwa kwa sababu kifungu cha sheria kilichotumika kuyafungua si
sahihi na kwamba hutumika pale ambapo sheria ziko kimya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...