Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi akimuhoji mmoja
wa Wamiliki wa kiwanda cha Afro African Company kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam
ambao ni wazalishaji na watengenezaji wa pombe mbalimbali aina ya viroba. Ofisi ya Makamu
wa Raisi inaongoza uendeshaji wa ukaguzi wa viwanda vyote jijini Dar es Salaam vinavyozalisha
na kutengeneza pombe kali(viroba) na kufunga kwa vifungashio vya plastiki.
Mwanasheria wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira NEMC , Heche Suguti akiwaonyesha
waandishi wa habari aina mojawapo ya pombe kali (kiroba) inayozalishwa na kampuni hiyo
pasipo kufuata kanuni za TFDA wala pasipo kuweka stika za TRA.
Mrundikano wa maboksi uliopo kiwandani hapo ambapo ndani yake tayari kumejazwa pombe za
aina mbalimbali aina ya viroba tayari kwa kuuza.
Mashine zinazotumiwa na kiwanda cha Afro African Company kuzalisha pombe kali aina ya
viroba pamoja na kutengenezea vifungashio vya plastiki vya kufungashia pombe hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...