Mafunzo
ya Ujasiriamali Awamu ya kwa Katika Msimu wa Pili wa Mradi wa Taasisi
ya Manjano Foundation ya Mafunzo ya Ujarisiamali kwa wanawake 32 kutoka
Mkoa wa Dar es Salaam Yamemalizika. Wanawake 32 wa mkoa wa Dar es salaam
ni miongoni mwa wanawake walionufaika na mafunzo ya ujasiriamali na
namna ya kupamba kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo
yaliendeshwa na wataalamu wa mambo ya Biashara wakishirikiana na maofisa
wa Taasisi ya Manjano.
Mafunzo
hayo yalilenga kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo
la ukosefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri ndani ya Tasnia ya
Urembo na vipodozi. Mafunzo hayo yatafanyika kwenye mikoa ya Dar es
Salaam, Mbeya,Mtwara,Tabora na Kigoma.

Baada
yanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation
itawaunganisha na Taasisi za Fedha zinazotoa mikopo bila riba waweze
kupata mtaji wa kununua bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha
kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa
Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.
Washiriki
walionufaika kwenye Mafunzo hayo wakiwa katika Picha ya Pamoja na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Africa na Mkurugenzi wa Taasisi ya
Manjano Foundation Mama Shekha Nasser.Wanawake wa mji wa Dar es Salaam
walionufaiki na mafunzo ya ujasiriamali na urembo wamemshukuru Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shear illusions na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano
Foundation kwa moyo wa kujitolea na kuwajali wanawake wengine hususani
wakazi wa Dar es Salaam .

Wakiongea
zaidi wanawake hao ambao wamepatiwa elimu ya biashara kutambua nafasi
yao katika jamii inayowazunguka pamoja na namba ya kupamba maharusi na
matumizi ya vipodozi. Wamemshukuru mama Shekha Nasser kwa moyo wenye
kuwajali na kuwabeba wanawake wenzake na kutoa elimu ya bure aliyokuwa
nayo kwa wengine ili waweze nao kujiongezea kipato na kupunguza ukali wa
maisha. Wamemshukuru na wameahidi kuyatumia mafunzo hayo kwa lengo la
kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira kwa wanawake na pia kujiongezea
kipato.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...