Na Mary Gwera - Mahakama

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu amemtembelea Kaimu Jaji Mkuu, ambapo amesisitiza juu ya ushirikiano kati ya Mahakama yake na Mahakama nchini. Rais huyo wa Mahakama ya Afrika, Mhe. Jaji Sylvain ORE` alimtembelea Mhe. Kaimu Jaji Mkuu mapema Machi 1, katika ofisi zake zilizopo Mahakama ya Rufani (T) jijini Dar es Salaam, ambapo lengo mojawapo la ujio wake ilikuwa ni kumpongeza Mhe. Kaimu Mkuu nchini kwa kuteuliwa kwake kushika nafasi hiyo.

Aidha mbali na kutoa pongezi, ujio wake pia umelenga katika kuendeleza mahusiano yaliyokuwepo wakati wa utawala wa Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Mohamed Chande Othman kwani Mahakama mdau mkubwa katika Mahakama hii. Mbali na kumtembelea Kaimu Jaji Mkuu, Rais huyo wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu alimtembelea pia, Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali.

Akitoa maelezo mafupi kwa niaba ya Kaimu Jaji Mkuu kwa mgeni huyo, Mhe.  Wambali alimueleza juu ya muundo wa Mahakama nchini na jinsi inavyofanya kazi ya utoaji haki nchini. Aliendelea kuongelea juu ya maboresho ya utoaji huduma ya haki kwa wananchi kwamba nia ya Mahakama ni kuwa na huduma ya Mahakama Kuu kila Mkoa ili kuwawezesha wananchi wa kila mkoa kupata huduma ya haki.

“Nia ya Mahakama ni kuwa na Mahakama Kuu katika kila mkoa, kwa sasa kuna zaidi ya mikoa 13 ambayo bado haina Mahakama Kuu, hivyo kwa Mwaka huu wa fedha Mahakama imepanga kuanza ujenzi wa jumla ya Mahakama Kuu nne, na tutakuwa tukifanya hivi kwa awamu kadri bajeti itakavyoruhusu,” alieleza Jaji Wambali.

Mbali na kukutana na Viongozi hao Wakuu wa Mahakama, Rais huyo wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu alipata wasaa wa kujionea muonekano wa kumbi za Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ya Tanzania. Rais huyo kutoka nchini Ivory Coast amechukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Rais wa Mahakama hiyo, Mhe. Jaji Augustino Ramadhani.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma (kulia), akimkaribisha Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu, Mhe. Jaji Sylvain ORE`, alipowasili ofisini kwake Mahakama ya Rufani (T).
Mhe. Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania (kulia) akifurahia jambo alipokuwa wakijadili jambo na mgeni wake.
Katibu wa Mhe. Kaimu Jaji Mkuu, Mhe. Elinaza Luvanda (kulia) akimuonesha kitu Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu, Mhe. Jaji Sylvain ORE` alipotembelea katika Ukumbi namba 1 wa Mahakama ya Rufani (T).
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania,Mhe. Ferdinand Wambali (kushoto) akimuonesha kitu Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu, Mhe. Jaji Sylvain ORE` alipokuwa katika Ukumbi namba 1 wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...