Wananchi wanaosafiri nje ya nchi wametakiwa kupata chanjo ya homa
ya manjano pale wanapohitaji kusafiri hususan siku kumi kabla ya
kusafiri na kupatiwa vitabu vipya.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu,Wizara ya afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati
alipotembelea hospitali ya Mnazi Mmoja jijini hapa kwa ajili ya kujionea
utaratibu wa kutoa chanjo pamoja na kubadilisha vitabu vipya vya
chanjo hiyo kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.
“chanjo hii ni muhimu hasa kwa zile nchi zenye changamoto za homa hii
ya manjano,kwahiyo ni vizuri kuwa na kinga kabla ya kusafiri nchi hizo ili
usije pata ugonjwa huo,’nilikua nchi ya Angola hivi karibu watu karibu
elfu mbili walipoteza Maisha”amesema Dkt.Mpoki
Hata hivyo kutokana na wingi wa watu kwa jiji la Dar es salaam na
uhitaji wa chanjo hiyo wamekubaliana kuweka taratibu ya kupunguza
watu kupoteza muda wa kufika mnazi mmoja kupata chanjo hiyo,hivyo
wameamua kupeleka huduma hiyo karibu na wananchi mahali walipo
“Muda ambao upo huku shughuli nyingi zinasimama,hivyo wataalam
watakaa na kuona mahali gani panafaa ili watu msipoteze muda wakuja
hadi huku mfano wa Ubungo wapate huko huko hivyo tunazitawanya
huduma hizi sehemu mbalimbali kwenye vituo vyetu vya huduma za
afya na taratibu zitatolewa”.
Kuhusu vitabu vipya vya chanjo Dkt. Mpoki amesema wanavyo vya
kutosha hivyo hamna haja ya wananchi kuwa na wasiwasi kama
watakosa vitabu kwani hakuna siku itatokea watanzania wote wakasafiri
kwa siku mmoja,na hivyo utaratibu mpya utatenganisha wale watu wa
kuchanja na wakubadilisha vitabu wasikae sehemu moja.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara Kuu ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya akikabidhiwa kitabu kipya cha kadi ya manjano na mmoja wa wauguzi wa Hospitali ya mnazi mmoja ya Jijini Dar es salaam. Katibu mkuu huyo mapema leo ametembelea kituo hicho kwa ajili ya kujionea wananchi wakipata chanjo pamoja na kubadilisha vitabu vipya vya njano hiyo ambapo mwisho wa zoezi hili ni mwezi huu.
Katibu Mkuu Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwaonesha kitabu kipya cha homa ya manjano ambacho inambidi mwananchi anayesafiri toka nchini Tanzania na kwenye nchi thelathini za Bara la Afrika anatakiwa awe amepata chanjo hiyo ili kumkinga na maambukizi ya homa ya manjano. Kitabu hicho (kadi) ni mbadala ya kile cha zamani ambapo kipo tofauti na ina lenga kudhibiti udanganyifu wa raia kupata kitabu bila kupata chanjo.
Dkt.Mpoki akiongea na wananchi waliofika kwenye kituo hipcho kwa ajili ya kupata chanjo ya homa ya manjano.
Wananchi waliofika kupata chanjo kwenye kituoni hapo wakisikiliza maelezo toka kwa watoa huduma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...