Mfuko wa Pensheni wa LAPF unatarajia kufanya mkutano wa tisa wa wadau tarehe 9 na 10 Machi, 2017 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC Jijini Arusha. Mgeni rasmi katika mkutano huu anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb).
 
LAPF imekuwa ikifanya mikutano hii ili kutoa taarifa za undeshaji wa Mfuko na kuwapa fursa wadau kutoa maoni mbali mbali ili kuboresha utendaji wa Mfuko. Aidha mikutano hii hufanyika ili kutekeleza maagizo ya mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa mifuko ya Hifadhi ya jamii nchini (SSRA).

Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Kuibua Fursa Endelevu za Ajira kwa maendeleo ya Hifadhi ya Jamii Tanzania”. Pamoja na mambo mengine kwenye mkutano huu mada mbali mbali zitawasilishwa ikiwemo mada inayohusu kauli mbiu jatwa hapo juu. Mada nyingine zitahusu Utendaji wa Mfuko kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016, Taarifa ya uwekezaji pamoja na Taarifa ya Hesabu za Mfuko kwa mwaka 2015/2016.

Kadhalika katika siku ya kwanza ya ufunguzi wa mkutano LAPF itazindua huduma ya Mkopo wa Kujikimu ijulikanayo kwa jina la Maisha Popote na LAPF) kwa kushirikiana na benki ya CRDB. Huduma hii imewanufaisha sana wanachama wa Mfuko wanaoanza ajira kwa kuwapa fursa ya kukopa mara tatu ya mshahara wao ili kukidhi mahitaji ya awali kama kulipa pango, nk kwa riba nafuu.

Vilevile siku ya ufunguzi wa mkutano tarehe 09 Machi, 2017 itakuwa ni siku ya maadhimisho ya figo duniani hivyo basi LAPF itatumia siku hii kuwapa fursa wadau wote watakao shiriki mkutano huu kupima figo kwa kushirikiana na wataalamu kutoka hospitali ya KCMC.

LAPF inatarajia kupata washiriki zaidi ya 600 katika mkutano huu kwa kuzingatia idadi ya waalikwa. Waalikwa wanaweza kuthibitisha ushiriki wao na kujisajili kwa kutembelea tovuti ya Mfuko www.lapf.or.tz . LAPF inawahamasisha wadau wote kujisajili kupitia tovuti ili kupunguza msongamano siku ya mkutano.

Aidha, siku ya pili ya mkutano tarehe 10 Machi, 2017, LAPF pamoja na washiriki wote wa mkutano wakiongozwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wanatarajia kushiriki katika mazoezi ya kutembea ikiwa ni kuunga mkono utekelezaji wa tamko la Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan.

Karibuni waalikwa wote kwa ustawi wa Mfuko.

  Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe (katikati), akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini kuhusu mkutano na wa tisa wa wadau wa LAPF utakaofanyika jijini Arusha Machi 9-10.kushoto ni  Ofisa Masoko na Mawasiliano, Rehema Mkamba na kulia ni Meneja Takwimu, Hadhari na Tathmini, Abubakar Ndwata.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe.
Pichani kulini ni Meneja Takwimu, Hadhari na Tathmini, Abubakar Ndwata akielezea mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kupitia mfuko huo wa Pensheni wa LAPF,Kushoto ni   Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo mapema leo,jijini dar
Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...