Na Catherine Sungura, WAMJW             
 Ujumbe wa wawekezaji toka nchini Misri umewasili nchini kufanya mazungumzo na serikali ya Tanzania kwa nia ya kujenga  viwanda vya dawa za binadamu zikiwemo za majimaji pamoja na zile za antibiotic.
Ujumbe huo ulikutana jana na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  pamoja na wawakilishi toka wizara Viwanda,Biashara na Uwekezaji na Kituo cha Uwekezaji cha Taifa (TIC) kwenye ofisi ndogo ya wizara ya afya, maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto iliyopo jijini Dar es Salaam
Ujumbe huo ulisema kuwa kiwanda walichokusudia kujenga nchini hapa kitazalisha  dawa za majimaji yaani “IV Fluids” pamoja na “antiobiotics” za aina mbalimbali  ikiwemo "Paracetamol IV” na dawa za kutibu Malaria
Aidha, walisema lengo lao ni kujenga kiwanda kikubwa ambacho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha dawa ambazo zitawahudumia watanzania pamoja na nchi za Afrika Mashariki na ya kati. Wawekezaji hao pia wanatarajia kuisaidia Tanzania katika uzalishaji wa chanjo ya ugonjwa wa homa ya Ini (Hepatics B na C ).
Kwa upande wake Waziri Ummy amewaahidi wawekezaji hao kuwasaidia katika mipango ya ujenzi huo na kutoa ushirikiano wa dhati katika kufanikisha viwanda hivyo vinajenga nchini kwa muda uliopangwa.
“Naelekeza kwa taasisi zote zitakazoguswa na uanzishwaji wa viwanda hivi watoe ushirikiano wa hali ya juu ili lengo hili lifikiwe,soko la dawa hapa nchini lipo naomba niwahakikishie hili”alisema waziri Ummy.
Waziri Ummy aliwaomba wawekezaji hao kuharakisha ujenzi wa viwanda huo na kujengwa ndani ya miezi kumi na nane kama walivyoahidi ili watanzania waanze kunufaika mapema. 
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika mazungumzo na Ujumbe huo wa wawekezaji toka nchini Misri kwenye ofisi ndogo ya wizara hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam
 Wawakilishi toka wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Kituo cha Uwekezaji cha Taifa (TIC) wakiwa katika mazungumzo hayo kwenye ofisi ndogo ya wizara ya afya, maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto iliyopo jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja  na Ujumbe huo wa wawekezaji toka nchini Misri  na Wawakilishi toka wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Kituo cha Uwekezaji cha Taifa (TIC) baada ya mazungumzo kwenye ofisi ndogo ya wizara hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...