Vurugur  zimeibuka wakati Wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) kupambana na  wenzao wanaosadikiwa kuwa wapinzani wao baada ya kundi hilo  kuvamia mkutano   na waandishi wa habari katika Hotel ya Vinna Hotel maeneo ya  Mabibo jijini Dar es salaam, na kuzua taharuki kubwa kwa waandishi wa habari na wakaazi wa eneo hilo.  Wanahabari kadhaa walijeruhiwa na mmoja kuharibiwa kamera yake ya video.
Mashuhuda wamesema watu kadhaa wasiojulikana walifika hapo wakiwa wamefunika nyuso zao kwa vitambaa huku wakiwa na silaha za jadi na kuanza vurugu.
Baada ya mkutano kuvurugika baadhi ya  waliokuja kufanya vurugu walikimbia huku wakikimbizwa na wanachi wenye hasira kali ambao walifanikiwa kumkamata mmoja wao na kumjeruhi  kwa kumkata maungio ya kisigino ya mguu wake wa kulia.
Juhudi za kuwapata wasemaji wa pande mbili hizo zinaendelea.
Taharuki  katika Hotel ya Vinna maeneo ya  Mabibo jijini Dar es salaam
 Mmoja wa watuhumiwa  wa uvamizi huo akiwa anapambana
 Mmoja wa watuhumiwa  wa uvamizi huo akiwa anapambana
 Mmoja wa watuhumiwa wa uvamizi akiwa chini ya ulinzi mara baada ya kudhibitiwa na na wananchi kisha kumkata mguu na kushindwa kutembea
Mtuhumiwa akiwa amekatwa mguu wa kulia akiugulia maumivu  baada ya kujeruhiwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...