Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama ameeleza kukamilika kwa maandalizi ya kuadhimisha sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zitakazofanyika Viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma, siku ya jumatano Aprili 26, 2017.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Aprili 22, 2017 katika Ofisi yake Dodoma.
“Nipende kuwaeleza Watanzania wote kuwa hadi sasa maandalizi ya kuifikia siku ya Maadhimisho ya Sherehe za Muungano tayari yamekamilika kwa kuangalia mambo yote yaliyopangwa katika ratiba ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli.”Alisema Waziri Mhagama.
Amesema sherehe hizo zitakuwa na upekee wa aina yake ukizingatia kuwa ni mara ya kwanza tangu Serikali ilipotimiza adhma yake ya kuhamia Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Bunge,Kazi, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na
waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53
ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika Mkoani Dodoma 26 Aprili
2017.Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Januari Makamba na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Jordan
Rugimbana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mhe.Januari Makamba akizungumza na waandishi wa habari leo Mjini
Dodoma kuhusu matukio mbalimbali yatakayokuwepo katika Maadhimisho ya Sherehe
za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika Mkoani Dodoma
26 Aprili 2017.Kushoto kwake ni Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi, Ajira na watu wenye Ulemavu
Mhe,Jenista Mhagama na mwishoni ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw.Jordan Rugimbana.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Jordan Rugimbana
akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya maandalizi ya
Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
yatakayofanyika Mkoani Dodoma 26 Aprili 2017 na kuwataka wananchi kujitokeza
kwa wingi.Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,
Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe,Jenista Mhagama na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Januari Makamba.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...