Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Mamlaka
ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya nchini inamshikilia
mmiliki wa kampuni ya Techno Net Scientific kwa kuingiza kemikali
bashirifu nchini zenye ujazo wa lita 6494 kwa kukiuka sheria na
taratibu.
Imeelezwa
kuwa, mmiliki huyo amekiuka sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za
kulevya namba 5 ya 2015 na ile usimamizi na udhibiti wa kemikali za
viwandani na majumbani, sheria ambayo inasimamiwa na Mkemia mkuu wa
Serikali.
Kamishna
Mkuu wa mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na dawa za kulevya Rogers Sianga
amesema kuwa, Kukamatwa kwa mmiliki wa kampuni hiyo, yenye makazi yake
eneo la mwenge kunatokana na taarifa walizopata kutoka kwa raia wema
mwezi uliopita waliowataarifu kuwa kampuni hiyo inaagiza kemikali
bashirifu, ambazo ni hatari kwa matumizi na zisiporatibiwa zinaweza
kutumika vibaya na kuleta madhara.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake leo, baada ya ziara fupi ya
kutembelea maghala mawili ya kampuni hiyo yanayotumika kuhifhadhia
kemikali hizo, Sianga amesema, uchunguzi wao umeonyesha kuwa, kampuni
hiyo inaagiza kemikali bila kibali.
“Tulichogundua
ni kwamba kampuni hii ya Tecno Net Scientific yenye makazi yake eneo la
mwenge, imeagiza kemikali nyingi ambazo ni bashirifu, kemikali
bashirifu ni kemikali muhimu kwa utengenezaji wa kawaida wa dawa za
binadamu lakini pia zikichepushwa zikiwa diverted zinaweza kutengeneza
dawa za kulevya za Heroine, Cocaine na nyinginezo ambazo huzalisha
kemikali taka zenye sumu ambazo zinaweza kuhatarisha afya za watu na
kuchafua mazingira.
Kamishna
Mkuu wa mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na dawa za kulevya Rogers
Sianga, akizungumza na Waandishi wa habari juu ya athari za Dawa hizo
ambazo zilikamatwa katika moja ya Maghala huko Mwenge
Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Kupambana na Dawa Bertha Mamuya akitoa ufafanuzi juu ya kemikali bashirifu zinavyoweza kuchepushwa kwa matumizi mengine
Kamishna
Msaidizi wa Mamlaka ya Kupambana na Dawa Bertha Mamuya akionesha
baadhi ya Maghala kwa ndani sehemu ya ghala ya kuhifadhi Dawa.
Kamishna
Msaidizi wa Mamlaka ya Kupambana na Dawa Bertha Mamuya akionesha ghala
la pili la kuhifadhi Dawa ambapo wamebaini kuwapo kwa dawa zilizomaliza
muda wake.
Sehemu ya nje ya jengo la kampuni ya Tecno Net Scientific ambalo lilitumika katika kutengenezea na kuhifadhi madawa hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...