Mafunzo hayo ambayo yamekwisha kuanza katika kata ya Nguvumali yanatarajiwa kuwafikia wanawake wajasiriamali 120 na baadae kuendelea kwenye maeneo mengine katika Jiji la Tanga.

Akizungumza juzi wakati akifungua mafunzo hayo,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi alisema mpango huo utasaidiakuwakomboa wanawake kiuchumi lakini pia kuwaandaa na ujio wa miradi mikubwa miwili mkoani hapa ikiwemo wa bomba la mafuta na kiwanda kikubwa cha kuzalishia saruji.

Alisema pia licha ya kuwapa uelewa masuala hayo lakini namna bora ya kuzitumia kwa malengo yatakayokuwa na tija fedha wanazokopa kutoka kwenye taasisi za kibenki kwani baadhi yao wanashindwa kutambua wazitumie vipi na kuzirejesha.

“Utakuta wakina mama wajasiriamali wanakopa fedha kwenye taasisi mbalimbali kwa malengo ya kufanya biashara lakini kutokana na kutokuwa na elimu hivyo wanaishia kuzitumia kwenye mambo mengine na kusababisha madeni “Alisema.
  Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi akizungumza na wakina mama wajasiriamali kwenye kata ya Nguvumali wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo ambayo aliyaandaa kwa ajili ya kukabiliana na fursa mbalimbali za kujiwekeza kiuchum ambapo mafunzo hayo yatafika kwenye kata 27 za Jiji hilo
 Baadhi ya wanawake wajasiriamali katika Kata ya Nguvumali Jijini Tanga wakiwa kwenye mafunzo hayo
WANAWAKE wajasiriamali Jiji la Tanga wanatarajiwa kunufaika na mafunzo ya kuwajengea uwezo katika utengenezaji na ubinifu wa bidhaa mbalimbali ili waweze kujikwamua kichumi jambo ambalo litasaidia kuondokana na utegemezi kwenye jamii.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...