Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo (kulia) akikata utepe kuzindua kisma cha maji mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.


 Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo (katikati) akisisitiza jambo kwa wageni waalikwa wakati akikabidhi kisima kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (Kushoto)  kwa ajili ya mahabusu ya watoto mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Padre Timotheo Maganga Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa Dar es Salaam.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto) akisisitiza jambo kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati akipokea kisima toka kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo (katikati) kulia ni Padre Timotheo Maganga.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (kushoto) akifungua bomba kuashiria kupokea kisima toka kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo kulia.
Picha na Eliphace Marwa - Maelezo.

Na Agness Moshi na Anthony Ishengoma- Maelezo.
Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam leo limekabidhi Kisima chenye thamani ya  Shilingi Milioni kumi na moja laki saba na themanini (Sh. 11,780,000/=) kwa Serikali ili kutatua tatizo la maji katika Mahabusu ya Watoto iliyoko Upanga jijini Dar es Salaam.

Akiongea katika hafla ya makabidhiano ya Kisima hicho Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo amesema lengo kuu la Mchango wa Kanisa katika ujenzi wa Kisima hicho ni kuonesha kuwa Kanisa haliko mbali na Serikali katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.

Alisema  Kanisa Katolitiki Tanzania linashirikiana na serikali katika juhudi zake za kuwaletea wananchi maendeleo bila kujali itikadi za kidini chama au kikabila ili kusudi wanapotoka kwenye vituo hivyo watambue wamesaidiwa  kutokana na mapenzi mema ya kanisa hilo kwa watu wote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...