Maendeleo
Bank leo imechezesha droo yake ya kwanza iliyotokana na kampeni ya
Maendeleo Pamoja na Wewe iliyozinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwezi Agosti
2017.
Promosheni hiyo ina malengo kadhaa;Kuwaweka wateja wake karibu kwa kutumia huduma mbalimbali za Maendeleo Bank Kuwajengea watanzania utaratibu wa kuweka akiba kwa njia ya kibenkiKukuza
utamaduni wa kujiwekea malengo ya muda mfupi na mrefu kwa kuweka fedha
kidogo kidogo katika akaunti ya WEKEZA ili kufanikisha malengo yao.
Kuwajengea wazazi utamaduni wa kuwawekea watoto wao akiba
Mkuu
wa Idara ya Fedha wa benki hiyo Bw. Peter Tarimo alisema “Draw yetu ya
Maendeleo Pamoja na Wewe awamu ya kwanza inahitimishwa leo kwa
kuchezesha draw ambayo itatupatia washindi mbalimbali ikiwemo tani za
simenti, kiwanja, mabati na ada ya shule”.
Draw
hiyo imeibua washindi wane (4) ambao walishinda kiwanja, mabati 64
,tani 3 za simenti pamoja na ada ya shule na kushudiwa na mwakilishi
kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Bw. Bakari Maggid.
Promosheni
ya Maendeleo Pamoja na Wewe inasitishwa kwa sasa kupisha zoezi za
uuzaji wa hisa za Maendeleo Bank na itaendeleo mara baada ya kuhitimisha
uuzaji wa hisa za benki hiyo.
Mkuu
wa Tehama na Uendeshaji Bw. George Wandwalo akibonyeza kitufe kuashiria
kuanza kwa droo iliyomuibua mshindi wa kiwanja Bi. Dora Olotu katika
droo iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni
mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bw. Bakari Maggid
Mkuu
wa Tehama na Uendeshaji Bw. George Wandwalo akizungumza na mteja wa
Maendeleo Bank kwa njia ya simu baada ya kuibuka kama mmoja wa washindi
waliopatikana katika droo iliyoashiria kumalizika kwa awamu ya kwanza ya
promosheni ya Maendeleo Pamoja na Wewe.
Mkuu
wa Kitengo cha Fedha Bw. Peter Tarimo akizungumza na waandishi wa
habari juu ya shindano na promosheni ya Maendeleo Pamoja na Wewe kabla
ya kuanza kwa droo hiyo Dar es Salaam leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...