Chama cha Mapinduzi kimesema kuwa kipo tayari kuingia katika uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Longido Mkoani Arusha mara baada ya kutangazwa kuwa jimbo hilo lipo wazi kutokana na maamuzi ya mahakama ya Rufaa iliyobainisha kuwa uchaguzi wa mwaka 2015 haukuwa huru na haki hivyo kufuta matokeo ya uchaguzi huo.

CCM imeeleza kuwa kulikuwa na matumizi yasiyostahili kutumika kujazwa matokeo ya Ubunge, kwa kutumia fomu namba 21c za kujaza matokeo ya Udiwani na kujaza matokeo ya Ubunge, badala ya kutumia fomu namba 21b jambo lililopelekea kufungua kesi ya kupinga ushindi wa Ubunge katika Jimbo hilo.

Kauli ya CCM imetolewa na Katibu Wa Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi Ndg Humphrey Polepole wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Polepole alisema kuwa vipo vyama vya siasa ambavyo kwa kawaida hulalamika kila vinaposikia kushindwa na mahakama kwa madai kuwa hakuna haki lakini vyama hivyo kila vinaposhinda vyenyewe husema mahakama imetenda haki.

Alisema kuwa kazi ya mahakama ni kutumia sheria zilizopo na kuamua juu ya malalamiko ya wananchi kwa kuhakikisha usawa mbele ya sheria kwa watu wote unatendeka hivyo maamuzi yaliyotolewa juu ya kuwa wazi kwa Jimbo la longido ni sehemu ya maamuzi huru na haki kwa mahakama ya Rufaa nchini.
Katibu Wa Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi Ndg Humphrey Polepole akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Katibu Wa Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi Ndg Humphrey Polepole katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.


Aliyekuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt Steven Kiruswa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Katibu Wa Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi Ndg Humphrey Polepole.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...