NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MUITIKIO wa waajiri kujisajili na kulipa michango katika Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) umekuwa wa kuridhisha hususani Mwezi Agosti, Meneja Matekelezo Bw. Victor Luvena amesema leo Agosti 31, 2017.
Itakumbukwa ya kwamba, tarehe 23 Julai 2017 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), alitoa siku 30 kwa waajiri wote nchini ambao walikuwa hawajasajili kuhakikisha wanajisajili katika Mfuko na wanawasilisha michango kwa wakati, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao na kama Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi inavyoelekeza.
“Kwakweli tunamshukuru Mheshimiwa Waziri kwa agizo alilolitoa kwani limetoa msukumo mkubwa, waajiri wengi wamejitokeza kutekeleza wajibu wao wa kisheria wa kujisajili na kuwasilisha michango katika Mfuko.” Alisema Bw. Luvena
K-VIS Blog ilishuhudia idadi kubwa ya waajiri wakiwa wamejitokeza leo Agosti 31, 2017 ambayo ndiyo siku ya mwisho kwa waajiri kutekeleza agizo la Mheshimiwa waziri, wakiwa wamejazana kwenye ofisi za WCF kujisajili na kuwasilisha michango, ambapo kazi hiyo ya kuwahudumia ilikuwa ikiongozwa na Meneja Matekelezo - WCF, Bw.Victor Ruvena.
Waajiri, wakihudumiwa na maafisa wa WCF, leo Agosti 31, 2017.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...