Video
Queen, Agnes Gerlda, maarufu kama Masogange (Kulia), akiwa na mpambe
wake wakitoka katika viunga vya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu ambapo
amepatikana na kesi ya kujibu katika tuhuma za matumizi ya dawa za
kulevya zinazomkabili mahakamani hapo uamuzi uliotolewa na Hakimu
Wilbard Mashauri.
Akisoma uamuzi huo baada ya shahidi Wa mwisho Wa upande wa mashtaka kumaliza kutoa ushahidi wake, hakimu Mashauri amesema, baada ya kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka ameridhika kuwa mshtakiwa ana kesi ya kujibu na kumtaka ajiandae kujitetea.

Mshtakiwa Msogange amedai kuwa atajitetea kwa kiapo na pia atakuwa na mashahidi watatu watakaofika mahakamani hapo kumtetea.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 12, mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...