Na Tiganya Vincent-RS –TABORA

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeiagiza Kampuni ya Jossam & co Ltd kuhakikisha inakamilisha barabara ilizopewa za Uledi na Mwenge katika Manispaa ya Tabora hadi kufikia mwishoni mwa Mwezi Septemba mwaka huu.

Agizo hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri baada ya kutembelea ujenzi wa barabara hizo zinazojengwa katika Kata ya Uledi na Isevya ili kujionea maendeleo na kuhakikisha kama mjezni amezingatia upana na urefu ullioandikwa katika makubaliano ya mkataba.

Alisema kuwa kiasi cha shilingi milioni 700 zilizopangwa na Manispaa ya Tabora kutumika kukamilisha mradi huo ni fedha nyingi ni vema Mkandarasi anayejenga mradi huo akahakikisha anajenga katika kiwango bora na kwa upana na urefu uliomo katika mkataba ili thamani ya pesa ionekane.

Mkuu huyo wa Mkoa aliwaagiza Watendaji wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanasimamia kwa karibu ujenzi wa barabara hizo unazingatia matakwa yaliyoelezwa katika Mkataba wa Ujenzi ili barabara hizo ziweze kutumika kwa muda mrefu bila kuharibika.

Awali Mhandisi Msaidizi kutoka Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Tabora Stephen Warioba alisema kuwa ujenzi wa barabara hizo unahusisha njia za waenda kwa miguu na ipaswa inamalize katika kipindi kilichoelezwa katika Mkataba.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mwl. Queen Mlozi alimwakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa atafuatilia kwa karibu ili kuhakikisha kuwa kazi inayofanyika katika eneo husika inazingatia mambo yote yaliyomo katika Mkataba na sio nje ya hapo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Bosco Ndunguru alisema kuwa baada ya ujenzi wa Mradi huu kukamilika kutakuwepo na zoezi la upandaji wa miti na maua kando kando ya barabara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...