Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Benard Paul 'Ben Pol ' maarufu kama kidume ameamua kuachia albamu yenye nyimbo 15, iitwayo The Best Ben Pol' itakayoanza kuwa mtaani keshokutwa ikiwa ni siku yake maalum ya kuzaliwa.

Mkali huyo wa R n B kesho kutwa Septemba 8 atasheherekea siku yake ya kuzaliwa huku akiachia albamu hiyo, ambayo itakuwa ikimfikisha miaka 8 toka kuanza kwake muziki wa kizazi kipya hapa nchini. 

Akizungumzia ujio wa albamu hiyo pamoja na wimbo wake mpya unaoitwa 'Kidume' ambao amemshirikisha mwanamuziki maarufu wa kike kutoka nchini Nigeria Chidinma, alisema kuwa uamuzi wake wa kutoa albamu ni kutaka kuendelea kuwa karibu na mashabiki wake ambao bila ya wao asingefika hapo alipo. 

Ben Pol alisema albamu mpya itatolewa rasmi kesho kutwa ambayo ni siku yake ya kuzaliwa na itakuwa na nyimbo 15, ikiwa na mchanganyiko wa nyimbo mbalimbali ambazo amezifanya kwa kushirikiana na wasanii wenzake wa muziki huo. 

"Mimi kama msanii nguli hapa nchini na Afrika Mashariki niliyefanya kazi yangu kwa miaka minane sasa, naona si vibaya kuendeleza muziki wangu kwa kutoa zawadi kwa mashabiki wangu kwa kutoa albamu yangu ya “Best of Ben Pol” ikiwa na nyimbo 15 nilizoshikirisha wasanii mbalimbali wkiwemo Darasa na Rama Dee” alisema Ben Pol. 

Alisema ameamua kufanya hivyo kwa sababu sasa ni mwaka wake wa nane katika safari yake ya muziki ikiwa ni pamoja na kuungana na mashabiki wake ambao wamekuwa wakimuunga mkono kila anapotoa nyimbo zake mpya. 

Albamu hiyo yenye mchanganyiko wa nyimbo mbalimbali ambazo amezifanya na kuweza kufanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya hapa nchini,ikiwa na nyimbo ijulikanayo kama Kidume, Tatu na Tuliza Boli, ambazo amewashirikisha Darasa na Rama Dee.

Katika kuhakikisha mashabiki wake wanapata vitu vizuri Ben Pol amehakikisha anafanya kazi nzuri katika nyimbo zake hizo mpya kama zile zilizopita ambazo mpaka leo zinaendelea kufanya vizuri na baadhi zikiwa Nikikupata, Maneno,Jikubali, Yatakwisha, Sophia, Moyo Mashine, Pete na Phone na kama msanii mwenye uwezo katika ukanda wa Afrika Mashariki anaamini kila mshabiki atapenda kupata albamu yake. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...