Na Bushiri
Matenda- MAELEZO
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga ameagana
na Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing.
Katika
hafla fupi iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Nje, Dkt.
Mahiga alimshukuru Balozi Dkt. Lu kwa kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali
ya nchi yake na Tanzania kwa muda wote alipokuwa nchini akitekeleza majukumu
yake.
Dkt.
Mahiga alimueleza Balozi huyo kuwa Tanzania na China ni ndugu kwani tangu
Tanzania ilipopata Uhuru imekuwa ikishirikiana na nchi hiyo yenye maendeleo
makubwa kiuchumi.
“Kwa
muda mrefu wizara zetu zimekuwa zikifanya kazi kwa karibu sana ambapo sasa
tumekuwa washirika wa karibu. Wewe Balozi umekuwa kielelezo tosha cha
kutekeleza tafsiri ya sera nzuri ya nchi yako kwa mataifa mengine ikiwamo
Tanzania” alisema Dtk. Mahiga.
Aidha,
Dkt. Mahiga alisifu utendaji wa balozi huyo kuwa wa ni wa kipekee kwani amekuwa
mnyenyekevu, msikivu na anafanya kazi zake kwa utaratibu na uhakika.
Alimshukuru
balozi huyo kwa jitihada zake za kuhakikisha watushishi wa wizara kuendelea
kupata mafunzo nchini China na kuomba kuendelea kushirikiana katika masuala ya
tafiti mbali mbali baina chuo cha Diplomasia nchini na vyuo vyao vya Diplomasia
vya China.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga
akimkabidhi tuzo ya kutambua mchango wake katika kuendeleza ushirikiano baina
ya Tanzania na China Balozi wa China aliyemaliza muda wake nchini Dkt. Lu
Youqing alipotembelea ofisi kwake leo Jijini Dar es Salaam.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...