Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi amesema uzoefu wa Sweden wa miaka mingi katika kuendesha serikali za Mitaa unaweza kuisaidia Zanzibar katika kipindi hiki cha ugatuzi.

Balozi Seif amesema hayo afisini kwake vuga wakati alipokuwa akizungumza na ujumbe wa watu wanane kutoka sweeden ukiongozwa na Spika wa Manispaliti ya Sundsvall Bibi. Arianne Sundman ambaye yupo nchini kwa ziara ya wiki moja.

Amesema Zanzibar hivi sasa inapitia katika kipindi cha mageuzi ya serikali za mitaa unaojulikana kwa jina la ugatuzi ili kuyafanikisha mageuzi hayo ni vyema kujifunza kutoka nchi mbali mbali zenye uzoefu.

Balozi Seif amefurahishwa na uhusiano uliopo kati ya Wadi ya Makunduchi na Manispaliti ya Sundsvall na kutaka uhusiano huo uimarishwe zaidi. Naye Spika wa manispaliti ya Sundsvall Bibi. Arianne Sundman amesema Manispaliti yake iko tayari kubadilishana uzoefu na Zanzibar katika sekta mbali mbali ikiwemo elimu.

Akielezea uhusiano uliopo kati ya Manispaliti yake na Wadi ya Makunduchi, Bi Arianne amesema ameridhishwa na uhusiano huo ambao unaimarika siku hadi siku. Wakati huohuo spika wa baraza la wawakilishi mh zubeir ali maulid amesema ujio wa wa ujumbe huo ni hatua muhimu ya kuimarisha uhusiano katika masuala muhimu ya maendeleo.

Akielezea shughuli zinazo fanywa ba baraza la wawakilishi mh zubeir amesema ni pamoja na kutunga shera, kupitisha bajeti, masuali na majibu pamoja na kupitisha mipango ya maendeleo. Nae spika wa manispaa ya sundsval ametoa shukrani kwa mapokezi mazuri waliyoyapata na kuahidi kuimarisha uhusiano kwa wawakilishi katika kubadilishana mawazo katika utekelezaji wa kazi zao za kila siku.

Mapema ujumbe huo ulipata nafasi ya kusikiza kipindi cha masulaa na majibu katika kiao cha baraza la wawakilishi kichoendelea na kutembelea sehemu mbali mbali za baraza ikiwepo chumba acha hansard. 
 Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na ujumbe wa Manispaliti ya Sundsvall Sweden
 Balozi Seif akitoa Zawadi ya kasha kwa Bibi Arianne Sundman, Spika wa Manispaliti ya Sundsvall, Sweden

picha ya pamoja na ujumbe wa Sundsvall ukiongozwa na Spika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...