NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MADABA.

WANANCHI wa Halmashauri ya mji wa Madaba, mkoani Ruvuma, wameipongeza serikali kwa kuwafikishia umeme kwenye eneo lao ambapo wamesema utabadilisha maisha yao.

Pongezi hizo zimetolewa Oktoba 11, 2017, kufuatia kukamilika kwa kazi ya kujenga njia ya kusafirisha umeme kwenye eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuweka mtandao wa nyaya (wiring), kwenye eneo hilo na kwenye nyumba za  wananchi kazi iliyokwenda sambamba na ufungaji wa  transofoma pozo.

Kwa sasa Serikali kupitia Shirika lake la Umeme, TANESCO inatekeleza mradi mkubwa wa umeme wa Makambako-Songea ambao unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa  msongo wa kilovolti 220Kv Transmision Lines na usambazaji umeme vijijini (Rural electrification), katika vijiji vya mkoa wa Njombe na Ruvuma ikiwa ni pamoja na kujenga vituo viwili vipya vya kupoza umeme, huko Madaba na Songea na upanuzi wa kituo kingine mjini Makambako.

“Nimefurahi sana eneo letu kupata umeme, kwa muda mrefu sana tumekuwa tukitegemea umeme wa solar, sasa nina matumaini makubwa nimeona kazi zinavyoendelea hapa za kuweka nguzo za umeme, kutandaza nyaya majumbani na kuweka transofa, na tumeambiwa tukae mkao wa kula kwani umeem utawaka muda wowote kuanzia hivi sasa.” Anasema  Rehema Maluwa, (pichani juu).
 Nyumba zikiwa na madishi ya tv kwenye Halmashauri ya mji wa Madaba mkoani Ruvuma ambazo bila shaka kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia fedha nyingi kutokana na matumizi ya jenereta kupata umeme lakini ujio wa umeme wa TANESCO utapunguza gharama za uendeshaji.
 Maendeleo ya ujenzi wa msingi wa kufungia mashine kituo cha Madaba, ukiendelea Oktoba 11, 2017.
  Maendeleo ya ujenzi wa msingi wa kufungia mashine kituo cha Madaba, ukiendelea Oktoba 11, 2017.
 Mafundi wa TANESCO kwa kushirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya India ya Kalpataru, wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa minara ya kupitisha laini za umeme wa 220kV huko Iboya, Njombe.
  Mafundi wa TANESCO kwa kushirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya India ya Kalpataru, wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa minara ya kupitisha laini za umeme wa 220kV huko Iboya, Njombe.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...