Ofisa Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akizungumza kuwakaribisha washiriki wa Kongamano la kimataifa la Wanawake na Fedha (hawapo pichani) kwenye hafla maalum ya 'cocktail' iliyoandaliwa na Benki ya Standard Chartered katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Biashara kati ya Mabenki, Bi. Heidi Toribio akishuhudia.
Ofisa Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akinyanyua glasi juu kuashiria uzinduzi wa hafla hiyo pamoja na washiriki wa Kongamano la kimataifa la Wanawake na Fedha (hawapo pichani) katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam.
Washiriki wa Kongamano la kimataifa la Wanawake na Fedha wakibadilishana mawazo kwenye hafla maalum ya 'cocktail' iliyoandaliwa na Benki ya Standard Chartered katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza jambo na Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na Wakati wa NMB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam. Katikati ni mmiliki wa mtandao maarufu wa Josephatlukaza.com, Josephat Lukaza akifuatilia mazungumzo hayo. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...