Waziri wa
Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe amezindua msimu wa 16 wa Mbio za
Kilimanjaro Marathon zinazodhaminiwa na
kampuni ya bia ya Kilimanjaro.
Dk Mwakyembe
amesema Kilimanjaro Marathon imejizolea umaarufu mkubwa kwa kuwa maandalizi
yake ni mazuri na kuweza kuongeza idadi
ya wakimbiaji mwaka hadi mwaka hali iliyofanya upatikanaji wa wakimbiaji wa
timu ya taifa kuwa raisi kupitia mashindano hayo ambayo kwa sasa yanatambulika
na chama cha riadha cha Dunia.
Aidha Waziri
Mwakyembe alitumia muda huo kuwashukuru wadhamini wengine ambao ni Tigo-21km,
Grand Malt 5km na wale wa meza za maji ambao ni pamoja na First National Bank,
Kilimanjaro Water, Diamond Motors Ltd, Kibo Palace, KK Security, Keys Hotel,
TPC Sugar, Simba Cement na KNAUF Gypsum.
kwa upande
wake Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Thomas Kamphuis amesema wanajivunia
kudhamini mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon ambazo zinakuwa kwa
kasi kubwa mwaka hadi mwaka na hii
inawapa moyo na ari ya kuendelea kuwa wadhamini wa mashindano hayo amabyo uleta
mataifa zaidi ya 40 pamoja.
Amesema
udhamini huu katika mbio za kilometa 42 na 5 kupitia Grand Malt, pamoja na
mambo mengine unalenga kuibua vipaji zaidi katika riadha na kuwataka washiriki
kujiandaa vizuri.
Meneja wa
Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli ametoa rai kwa washiriki kuhakikisha
wanajiandikisha mapema li kuepuka usumbufu dakika za mwisho na kutoa mfano wa
mwaka huu ambapo namba za ushiriki zilikwisha kutokana na watu wengi zaidi
kujitokeza mwishoni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...