Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akisikiliza Maelezo kutoka kwa washiriki tofauti wa Mkutano Mkuu wa Maafisa Ustawi wa Jamii nchini katika moja ya eneo la maonesho ya masuala yahusuyo Ustawi wa Jamii wakati wa Ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika UDOM Mjini Dodoma.
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi akipokea moja ya kitabu kinachoelezea masuala mbalimbali ya Ustawi wa Jamii kutoka kwa mshiriki wa Mkutano Mkuu wa Maafisa wa Ustawi wa Jamii nchini wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Maafisa wa Ustawi wa Jamii nchini uliofanyika UDOM Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa TASWO Dkt. Zena Mabeyo akitoa salamu za wananchama wa TASWO kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(kulia waliokaa) wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Maafisa wa Ustawi Jamii nchini uliofanyika UDOM Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Taasisi ya JSI Dkt.Tuli Tuhuma akitoa maelezo kuhusu kazi za Taasisi yake kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(kulia waliokaa) katika kuleta ufanisi wa kazi za Ustawi wa Jamii nchini wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Maafisa Ustawi wa Jamii nchini uliofanyika UDOM Mjini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...