Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi, Mh. Abdalah Hamisi Ulega ameitaka Halmashauri ya wilaya Mkuranga kushirikiana na wananchi kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji ili kupunguza migorogoro ya wakulima na wafugaji.

Akizungumza na watendaji wa Halmashauri pamoja na kamati ya ulinzi na usalama katika ziara yake ya wilayani Mkuranga mkoani Pwani alisema tatizo la wakulima na wafugaji ni changamoto kubwa kwahiyo ni muhimu kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji ili wasizagae hovyo.

Ametaka maafisa mifugo wasikae maofisini bali waende kutoa huduma vijijini na kuwasiliza wananchi kero zao.Ulega amesema vikundi vya wafugaji wakina mama na vijana vipewe kipaumbele, vitambuliwe na kudhaminiwa kwenye utoaji mikopo kwa ajili ya kuinua kipato na kuongeza pato la taifa na la mtu mmoja mmoja

"Tunahitajika tutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji, na hii ni changamoto tunayotakiwa kuifanyia kazi hatupaswi kuwaacha wafugaji wakihamahama" amesema Ulega. 

Aidha alisema kuwa Halmashauri inatakiwa kufanya utafiti na kupima ardhi ambayo watawatengenezea miundombinu bora kwa ajili ya wafugaji. Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya mkuranga, Filiberto Sanga alisema kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni ardhi, wananchi wanauza ardhi kiholela kiasi kwamba wanakosa maeneo ya kilimo hivyo amewataka wananchi kutouza ardhi hovyo. 

Sanga alisema kuwa agizo la naibu waziri wamelipokea japokuwa wanauhaba wa ardhi lakini wameanisha baadhi ya maeneo yaliyopo tarafa ya Mkamba ambayo watayafanyia utafiti kwa ajili ya wafugaji. 
Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega akizungumza na watendaji wa Halmashauri pamoja na kamati ya ulinzi na usalama kuhusu kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji ili kupunguza migorogoro ya wakulima na wafugaji mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, filiberto Sanga akizungumza katika mkutano huo amewataka wananchi kutouza ardhi hovyo ili kupunguza migogoro ya ardhi pamoja na kuwa na maeneo ya kilimo. 
Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi ,Abdalah Ulega akizungumza na viongozi mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi alipokutana nao na kufanya mazungumzo kuhusu usawa na wajibu wa kila mtu ili kufikia malengo ya taifa kiujumla mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi ,Abdalah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama hicho leo mkoani Pwani.(Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...