Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Asasi za kiraia na wadau wa elimu pamoja na Afya wameiomba serikali kutatua changamoto za watoto wa kike zinazofanya washindwe kutimiza ndoto mbalimbali ikiwemo ndoa za utotoni zinazotokana na mila potofu zinazoendelea katika jamii.

Akizungumza na waandishi habari wakati akimkabidhi mapendekezo ya wadau kwa  Afisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Dora Meena,Meneja wa Miradi ya Utetezi na Sera wa Taasisi ya Healthy Promotion (HDT), Gresmo Mutashobya amesema kuwa wasichana wenye umri kati 10 hadi 19 takribani ya milioni 600 duniani , Tanzania takribani ya asiliamia 18 ya ripoti ya 2016 inaonesha kuwa idadi ya udahili kwa watoto wa kike kwa shule za msingi ilizidi kwa wavulana kwa asilmia 0.1 na udahili wa shule za sekondari ilizidi kwa asilimia 6.1.

Amesema miaka 10 iliyopita wasichana 550,000 walikatishwa masomo baada ya kupata ujauzito hali iliyosababisha watoto wengine kuathrika katika maisha yao yote kutokana na kukosa elimu.

Mutashobya ameiomba Serikali kutengeneze mazingira ya usawa ambayo yatahamasisha elimu kwa mtoto wa kike ikiwa ni pamoja na kuondoa vizuizi katika elimu kwa mtoto wa kike pamoja na kufanya mapitio ya sheria na sera, ili kufanya mabadiliko ya sera na sheria zinazopalilia mila potofu, unyanyasaji na ndoa za utotoni kwa ubadilishaji wa sheria ya ndoa ya mwaka 1977 za mtoto wa kike kuolewa miaka 14.

Amesema changamoto zingine kwa wazazi wanatakiwa kuzingatia malezi ya watoto wa kike kuwa mstari wa mbele kuondoa dhana ya upendeleo wa kijinsia, pamoja na kuwatia moyo watoto wa kike kuwa wavumilivu kutoingia katika mahusiano ya kimapenzi kabla ya wakati.
.Meneja wa Miradi ya Utetezi na Sera wa Taasisi ya Healthy Promotion (HDT), Gresmo Mutashobya akizungumza juu ya asasi za kiraia zinavyofanya kazi katika kufanya utetezi kwa mtoto wa kike ili aweze kufikia ndoto zake katika kilele cha Maadhimisho ya Mtoto wa Kike ambayo hufanyika Oktoba 10 kila mwaka, iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Vijana Ofisi Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Dora Meena akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Mtoto wa Kike iliyofanyika jana  jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Miradi ya Utetezi na Sera wa Taasisi ya Healthy Promotion (HDT), Gresmo Mutashobya akimkabidhi mapendekezo ya asasi za kiraia juu changamoto za mtoto, Afisa wa Vijana Ofisi Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Dora Meena katika kilele cha Maadhimisho ya Mtoto wa Kike ambayo hufanyika Oktoba 10 kila mwaka, iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wanaasasi na waandishi wakisikiliza taarifa ya kilele cha maadhimisho ya siku mtoto wa kike Duniani.
Mbunge wa Afrika Mashariki Mhandisi Pamela Massay akizungumza katika maadhimisho ya siku Mtoto wa kike iliyofanyika jana  jijini Dar es Salaam.
Wanaasasi wakiwa na wameshika ujumbe mbalimbali wa watoto wa kike kuweza kufikia ndoto zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...