Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi zao ili kuleta mabadiliko makubwa kwa wakulima.

Akiongea katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Uthibiti wa Mbolea (TFRA) jana na kuwahusisha Watumishi wote wa Taasisi hiyo, Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi hao kuwa na malengo na mpango kazi ambao kila mtu atautekeleza  na atapimwa kutokana na mpango kazi huo.

 Hata hivyo Dkt. Mwanjelwa amewapongeza  kwa namna wanavyotekeleza majukumu yao kwa sasa, hususan katika zoezi la uagizaji wa mbolea kwa mfumo wa pamoja (Bulk Procurement System) ambao umechangia kwa kiasi kikubwa mbolea hiyo kumfikia mkulima kwa bei nafuu.Pamoja na pongezi hizo Naibu Waziri, Dkt. Mwanjelwa ameitaka  TFRA  kuongeza bidii katika utendaji wao wa kazi na kuhakikisha kuwa wanaondoa kero zinazowakabili Wakulima.

Aidha ameitaka Mamlaka ya Uthibiti wa Mbolea kuhakikisha kuwa mambo matatu muhimu yanazingatiwa ambayo ni upatikanaji wa mbolea (Availability) ufikishaji wa mbolea karibu zaidi kwa Wakulima (Accessibility) na kwa bei ambayo wakulima wanaweza kumudu kuinunua (Affordability) .“Mhakikishe mbolea inakuwepo nchini kote na wakulima wanapohitaji inapatikana na iwe kwa gharama ambayo Mkulima anaweza akanunua. “Amekaririwa, Naibu Waziri.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa mamlaka hiyo bwana Lazaro Kitandu amemshukuru Naibu waziri kwa kuwatembelea na kuwatia moyo katika utendaji kazi wao na kumhakikishia kwamba TFRA imejipanga vizuri kupambana na changamoto za baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu hasa katika kuzingatia bei elekezi ya mbolea.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza viongozi pamoja na wafanyakazi katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Uthibiti wa Mbolea (TFRA)
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akipata maelezo kuhusu sampuli ya mbolea aina ya DAP kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mbolea (TFRA) Bwana Lazaro Kitandu  alipotembelea ofisi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...