Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha amesema wanafunzi wa elimu ya juu wanatakiwa kupata mikopo kwa muda mwafaka ili waanze kuhudhuria masoma yao.
Nasha ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea bodi ya Mikopo ya Elimu Juu jijini ambapo amesema hataki kuona wanafunzi wenye vigezo vya kupata mkopo wanakosa.
Amesema fedha iliyoidhinishwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu wale wanaostahili kwa sifa na vigezo ni sh. Bilioni 427 na na robo ya fedha hizo ambayo imeshatumwa katika katika akaunti ya bodi ya mikopo ni sh.milioni 147.
Ole Nasha amesema kuwa, kufikia Ijumaa ya Wiki hii mikopo hiyo iwe imeshakwenda kwa walengwa na rufaa za wale ambao hawajapatiwa huku wana sifa za kupata mikopo hiyo, kufikia Novemba 30 ziwe zimeshakwisha.
“Fedha zimetoka kwa wakati hatutaki wanafunzi wacheleweshewe lengo la serikali ni kuhakikisha wanafunzi hawapati usumbufu” amesema Ole Nasha.
Amesema ili kuondokana na wanafunzi hewa fedha za wanafunzi wanaorudia mitihani zipelekwe katika vyuo husika na zile zitazobaki zirudishwe.
Aidha, Ole Nasha ameiomba bodi kuwatangaza katika vyombo vya habari wadaiwa sugu ambao wamekuwa wakichelewesha urejeshaji wa mikopo kuweza ili kuwasukma waweze kulipa na baadae bodi iweze kujiendesha.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya elimu ya Juu, Abdul-Razaq Badru amesema kuwa wamejiwekea mikakati mbalimbali katika bodi ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi
Amesema moja ya mikakati ni kuboresha mifumo ya Tehama katika kuweza kutunza kumbukumbu mbalimbali itayoweza kurahisisha shughuli za bodi kufanya kazi ya kuwahudumia wanafunzi katika utoaji wa mikopo.
Aidha amesema bodi inatarajia kuongeza uwigo wa urejeshaji mikopo kwa wale walionufaika na mikopo hiyo.
Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia , William Ole Nasha akipata maelezo kwa Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Ignatus Oscar wakati alipotembelea bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia , William Ole Nasha akipata maelezo kutoka Kaimu Mkurugenzi wa Upangaji Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Nchini , Deus Shangala jinsi wanavyopanga mikopo,wakati Naibu Waziri wa Elimu, alipotembelea bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia , William Ole Nasha akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kutembelea Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Nchini, Abdul-Razaq Badru akizungumza juu ya mikakati ya bodi hiyo kwa Naibu Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...