Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji wa Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha,akiwataka kuwa watulivu wakati suala la mgogoro kati yao na hifadhi likiwa linashughulikiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Naibu Waziri Ulega ameeleza hayo jana katika mkutano na wafugaji hao uliofanyika kwenye Kata ya Ololosokwan wilayani humo.

“Wakati tunamsubiri Waziri Mkuu atoe maelekezo naomba msiharibu hali ya hewa, hii ndiyo rai yetu kama Serikali,ama kama kuna yeyote anayepinga jambo hili? Aliwauliza wafugaji hao na kujibiwa hakuna na wote wapo pamoja na Serikali.

“Hatua hii itaturahisishia sisi kwa sababu wizara inaliangalia jambo hili kwa ukaribu kutokana na sehemu kubwa ya nchi, wafugaji wamekuwa na malalamiko makubwa sana ikiwemo kufilisi mifugo yao pindi inapoingia hifadhini na kusababishiwa umasikini,”amesema Ulega.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka alimweleza Ulega kwamba ukosefu wa malisho ni mojawapo ya changamoto inayowakabili wafugaji hao kutokana maeneo machache yaliyopo.

Hata hivyo, Ulega alihaidi kulishughulikia changamoto hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa pamoja watatafuta mashirika kwa ajili kuangalia namna ya kuboresha malisho hayo ili kuleta ahueni kwa wafugaji hayo.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akisalimiana na wazee wa Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mmoja wa wafugaji akieleza jambo mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

 Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka akizungumza na wananchi wa kata ya Ololosokwan mkoani Arusha.
Wananchi wa kata ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha,wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,alipokuwa akizungumza nao kuhusiana na mambo mbalimbali ikiwemo mgogoro wa mpaka na hifadhi. 

Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii,Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...