Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Dkt. James Kilaba (kulia) alipofanya ziara TCRA kuangalia namna taasisi hiyo inavyosimamia maudhui ya vyombo vya habari nchini leo Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Posta TCRA Bibi. Cecilia Mkoba (kulia) akimuelezea Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) namna mawasiliano zamani yalivyokuwa yakifikishwa kutoka eneo moja kwenda eneo lingine alipotembelea makumbusho ya mawasiliano leo wakati wa ziara yake TCRA Jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Dkt. James Kilaba (katikati) akizungumza alipomtembeza Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza kuangalia gari lililofungwa mtambo wa kusimamia masafa ya redio nchini wakati wa ziara yake TCRA leo Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) akikagua ofisi za Idara ya uhariri na uchapishaji alipotembelea ofisi za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kukagua na kuona shughuli zinazofanywa na Baraza hilo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mtendaji BAKITA Dkt. Suleiman Sewangi 
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akipokea kamusi kutika kwa mtumishi wa BAKITA Bibi. Wema Msigwa alipofanya ziara katika ofisi za BAKITA leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji BAKITA Dkt. Suleman Sewangi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...