Chama cha Wanayansi wa Elimu Bahari ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi (WIOMSA) kimeandaa mashindano ya kazi za sanaa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za Tanzania. Dhima ya mashindano hayo ni: “Umuhimu wa Mazingira ya Pwani na Bahari kwa Tanzania”. Chora, paka rangi, tumia program za kompyuta za uchoraji au eleza mawazo yako hayo kwa kutunga wimbo.   

Vigezo na Masharti ya Kushiriki 
Uwasilishaji wa ubunifu huo unaweza kufanyika kwa michoro (zikiwemo katuni/vibonzo) au utunzi wa nyimbo. Mwanafunzi anaweza kuwasilisha kazi moja kwa kila njia ya uwasilishaji. 
i) Majina na mawasiliano. Andika jina lako, tarehe ya kuzaliwa, jinsia, anuani kamili ikiwemo namba ya simu na jina la shule. 
ii) Maelezo: Andika maelezo ya sentensi moja kuhusiana na kazi yako ya sanaa.

Tuzo:
Tuzo zitatolewa kwa washindi watatu wa mwanzo kwa kila kundi
i. Cheti 
ii. Seti ya vitabu vya shule 
iii. Pesa taslimu: Mshindi wa kwanza 1,000,000/- Mshindi wa pili 500,000/- na Mshindi wa tatu 300,000/-

Mfumo wa uwasilishaji: 
i. Michoro: iwe kwa rangi nyeusi na nyeupe au rangi mbalimbali na zichorwe kwenye karatasi ya ukubwa wa A4 (iwe ni ukurasa mmoja tu). Kwa kuwasilisha kupitia mtandao utapiga picha kwa scanner na kuipakia kwenye mtandao kwa muundo wa jpg au pdf).
ii. Utunzi wa muziki: urekodiwe kwa kuimbwa bila vyombo (acapella) au na vyombo vya muziki (uimbwe kwa muda wa kati ya dakika 1 - 3 tu uhifadhiwe kwenye kwenye mfumo wa mp3 au mp4 kwa ajili ya kupakia mtandaoni au kuwekwa kwenye CD au flash drive kwa ajili ya kutumwa kwa njia ya posta.

Kazi zote za sanaa ziwasilishwe kabla ya Jumanne 31 Oktoba 2017 kupitia: 
au
2. Njia ya posta kwenda: 
WIOMSA 
S.L.B 3298, 
Zanzibar
au
3. Namba ya whatsApp: 0767 254 887

Kwa maelezo zaidi wasiliana kupitia:
 +255 24 2233472 / +255 24 2234597 au secretary@wiomsa.org

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...