Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara maalum kukagua masuala mbalimbali ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro sambamba na kuzungumza na viongozi wa Mamlaka hiyo kwenye eneo la makao makuu yake yaliyopo ndani ya hifadhi. 

Katika ziara hiyo, Waziri Dkt. Kigwangalla ameweza kupokea kupokea maoni na masuala mengine ya kuendeleza Mamlaka hiyo ya Ngorongoro. Waziri yupo Ngorongoro kwa muda wa siku mbili ambapo pia amepata kutembelea maeneo ya hifadhi yenye migogoro na wafugaji.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akipokelewa na viongozi wa Ngorongoro wakati alipowasili kwenye makao makuu ya hifadhi ya Ngorongoro leo Oktoba 25, 2017.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa viongozi wa hifadhi hiyo wakati alipowasili kwenye makao makuu ya hifadhi ya Ngorongoro leo Oktoba 25, 2017.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa mhifadhi wa Ngorongoro wakati alipowasili kwenye makao makuu ya hifadhi ya Ngorongoro leo Oktoba 25,2017
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akisikiliza maoni kutoka kwa viongozi wa hifadhi ya Ngorongoro wakati alipowasili kwenye makao makuu ya hifadhi ya Ngorongoro leo Oktoba 25,2017.
Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Freddy Manongi akizungumza wakati wa kumkaribisha Waziri wa Maliasili Dkt.Kigwangalla alipowasili hapo mapema leo kwa ajili ya kupata maelezo na ya kina namna ya uendeshaji na masuala mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...