Na Karama Kenyunko, Glogu ya Jamii.
MAHAKAMA
Kuu Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, kwa kushirikiana na wazee wa
baraza wa mahakama hiyo kesho wanatarajia kutoa muhtasari wa kesi ya
mauaji ya bila kukusudia inayomkabili msanii wa filamu nchini, Elizabeth
Michael maarufu kama Lulu anayedaiwa kumuua msanii mwenzake marehemu
Steven Kanumba.
Jaji Sam Rumanyika amesema kuwa muhtasari huo
utasaidia wazee wa baraza kupitia shauri hilo na kuamua kama Lulu
anahatia ama la. Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa utetezi kufunga
ushahidi wao kwa Stafu Sajenti, E 103 Nyagea (53) kusoma maelezo ya
ushahidi ya Josephine Mushumbus ambayo aliyarekodi.
Maelezo hayo
yalisomwa baada ya wakili wa utetezi, Peter Kibatala kumueleza Jaji
Rumanyika kuwa wanaomba askari huyo ayasome maelezo ya Mshumbus ambaye
ni shahidi wao pili kwa sababu yeye ndiye aliyemuandikia na yuko mbali
hawezi kupatikana kwa urahisi.
Akisoma maelezo hayo, amesema
kuwa anamfahamu Mushumbus na ndiye aliyeandika maelezo yake ya ushahidi.
Amesema kuwa katika maelezo hayo Mushumbus alijitambulisha kuwa ni
Daktari, ana miaka (46) Mkazi wa Bunju National Housing na aliyaandika
maelezo hayo April 23, 2012.
Akimnukuu Mushumbus, askari huyo
alisoma kuwa;MShumbusi alimwambia kuwa yeye ni mmiliki ya clinic ya
precious inayotoa tiba mbadala iliyopo katika jengo la Mawasiliano
barabara ya Sam Nujoma.
Katika clinik yake alikuwa akitibu wateja
wa aina mbali mbali akiwemo marehemu Steven Kanumba ambaye alimfahamu
tangia Agosti mwaka 2011 alipofika katika clinic yake hiyo kwa Mara ya
kwanza kwa ajili ya kutoa sumu mwilini, na kuanzia hapo akawa na mazoea
ya kwenda hapo clinic kwa ajili ya huduma hiyo.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...