Mkazi wa Iringa, Alex Kalinga (26) amejishindia kitita cha sh milioni 161 kwa kubashiri kwa usahihi mchezo maarufu kwa ‘Perfect 12’ unaondeshwa na kampuni ya mchezo wa kubahatisha ya M-Bet.

Kalinga alikabidhiwa kitita chake jana na Afisa Habari wa Kampuni ya M-Bet, David Malley kwa kushirikiana na Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Catherine Lamwai.

Malley alisema kuwa Kalinga alifanikiwa kubashiri sahihi jumla ya mechi 12 kati ya 17 na kuwa mshindi wao wa droo ya 17 tokea kuanzishwa kwa mchezo wa Perfect 12.Alisema kuwa serikali imejipatia jumla ya Sh milioni 29 kutoka kiasi hicho cha fedha ambacho ni asilimia 18 kwa mujibu wa sheria.

“Ni faraja kubwa kuona kijana mwenye umri wa miaka 26 akishinda mamilioni ya fedha kwa kutumia kiasi cha She elfu moja tu, hii imedhihirisha kuwa M-Bet ni nyumba ya mabingwa, tunawaomba mashabiki wa soka kuendelea kucheza mchezo wetu ili kujishindia fedha,” alisema Malley.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Kalinga alisema kuwa hakuamini taarifa ya kushinda mchezo huo mara baada ya kupokea simu ya kujulishwa kushinda.

“Nina furaha sana, mimi ni fundi wa kuchomelea mageti ya chuma, sikuwa na kipato kikubwa pale Iringia Mjini, nitaanza kujenga nyumba na kufungua kiwanda cha kuchomelea na nyingine kusaidia familia yangu,” alisema Kalinga.

Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Catherine Lamwai aliwashukuru M-Bet kwa kuendelea vyema na shughuli zake mbali ya kuwazawadia washindi mara kwa mara.
 Afisa Habari wa Kampuni ya M-Bet, David Malley (katikati) akimkabidhi hundi mshindi wa mchezo wa Perfect 12 Alex Kalinga (kulia) ambaye amejishindia kitita cha sh milioni 161. Kuliakushoto ni Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Catherine Lamwai.
Mshindi wa mchezo wa Perfect 12 Alex Kalinga 'akipozi' na mfano wa hundi mara baada ya kukabiziwa jana. Kalinga alijishindia kitita cha sh milioni 161.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...