Tanzania na China wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika maeneo mbalimbali kama njia
mojawapo ya kupambana na uhalifu wa kimataifa ambao umekuwa ukiisumbua dunia.
Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya kufanyika mazungumzo kati ya Waziri wa Katiba na Sheria Prof.
Palamagamba Kabudi na mgeni wake Naibu Waziri wa China mhe. Zhao Dacheng ambae yuko nchini kwa
ziara ya siku nne nchini.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo, Prof.Kabudi ameyataja makosa ya kimataifa
ambayo wamekubaliana kuwa ni makosa ya kimtandao,utakatishaji fedha, usafirishaji binadamu na
mengineyo ambayo yamekuwa yakiikabili dunia kwa wakati huu.
Prof.Kabudi pia amesema kwamba wamekubaliana kuimarisha ushirikiano kayika eneo la msaada wa
kisheria kwa watu wenye uhitaji ambapo China pia watajifunza kutoka kwa Tanzania katika eneo hilo
ambalo Inataka kuwa na sheria yake kama ilivyofanya Tanzania.
Viongozi hao pia wamekubaliana kushirikiana katika eneo la mafunzo ili kuwaongea ujuzi na uwezo
watendaji wao kupitia semina za kimataifa au mafunzo maalum ili kubadilidhsna uwezo na uzoefu katika
eneo la usimamizi wa sheria nchini.
Tanzania na China pia wamekubaliana kushirikiana katika eneo la Mahakama ikiwa ni pamoja na
usimamizi na uendeshaji wa Magereza nchini.
Awali akizungumza katika kikao hicho Naibu Waziri wa China Mhe. Dacheng alisema Tanzania ni moja ya
nchi marafiki wa dhati wa China urafiki ambao uliasisiwa na viongozi waandamizi wa nchi hizo.
Alisema ziara yao nchini inafungua milango mipya ya ushirikiano baina ya China na Tanzania na
kuongeza kuwa itazidi kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo.
Amesema anaamini kuwa Wizara yake imedhamiria kuisaidia Tanzania katika sekta ya Sheria ili isonge
mbele kama ilivyofanikiwa China na kuongeza kuwa wao pia wataitumia nafasi hiyo kujifunzakatima
maeneo ambayo Tanzania imepiga hatua kama eneo la msaada wa sheria kwa watu wake.
Naibu Waziri huyo wa Sheria wa China yuko nchini kwa mwaliko wa Waziri wa Katiba na Sheria wa
Tanzania Prof. Kabudi, anatarajiwa kutembelea Shule Kuu ya Sheria ya Chio Kikuu chabDar es salaam na
Chama cha Wanasheria Tanganyika na Desemba Mosi ataelekea visiwani Zanzibar ambako atakutana na
Jaji Mkuu wa Tanzania na viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof.Palamagamba Kabudi wa pili kushoto akizungumza na ugeni wa Naibu Waziri wa Sheria wa China mhe. Zhao Dacheng katika ukumbi wa mikutano jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Sheria wa China mhe. Zhao Dacheng watatu toka kulia na ujumbe wake wakiwa katika ukumbi wa mikutano jijini Dar es salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Kabudi aliekaa katikati akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Sheria wa China mhe. Zhao Dacheng wa pili kushoto wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mazungumzo yao jijini Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...