Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

JALADA la kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani milioni 3.7, sawa na Sh.bilioni nane, dhidi ya vigogo wanne wa Kampuni ya Six Telecoms Limited na kampuni yenyewe limetua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP).

Mwendesha mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.

Hatua hiyo imefika baada ya Kishenyi kuieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Kutokana na taarifa hiyo, wakili wa utetezi Alex Mgongolwa aliomba kujua upelelezi dhidi ya kesi hiyo umefikia wapi.

"Mheshimiwa, jalada la kesi hii liko kwa DPP, tunaomba tarehe nyingine ya kutajwa", amedai Kishenyi.

Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 19, mwaka huu kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mhandisi  na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya  Six telecoms,   Hafidhi  Shamte, Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mwanasheria na Mhadhiri na Mkurugenzi wa hiyo kampuni Dkt ,Ringo Tenga,  Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms Limited.

Wote kwa pamoja wanadaiwa kuhujumu miundombinu ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa kutoza garama chini ya kiwango, kushindwa kulipa ada za udhibiti na kutakatisha 3,282,741.12.

Pia washtakiwa hao wanadaiwa kuisababishia TCRA hasara ya USD 3,748,751.22, sawa na Sh 8 bilioni  za kitanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...