Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa jana usiku amefanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam na kubaini mawakala wa meli wanaotoa huduma katika bandari hiyo hawafanyi kazi saa 24 kama Serikali ilivyoelekeza.
Prof. Mbarawa ameiagiza Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA) kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria kwa mawakala wote waliokiuka agizo la Serikali la kutoa huduma bandarini kwa saa 24.
"Kati ya Mawakala wa Meli nane ambao tumewatembelea usiku huu ni wakala mmoja tu ndiye tuliyemkuta akitoa huduma kwa saa 24 hivyo SUMATRA katika kipindi cha siku saba hatua za kinidhamu na kisheria zichukuliwe kwa wote wanaokiuka utaratibu huu na nipewe ripoti ya hatua zilizochukuliwa," alisema Waziri Prof. Mbarawa.
"Katika ukaguzi huu tumegunduwa kuwa mawakala wengi wanaacha watoa huduma wasiostahili, wakiwemo walinzi kufanya kazi nyakati za usiku ambao hawawezi kutoa huduma inayostahili usiku na kuendelea kutoa huduma asubuhi jambo ambalo sio sahihi," amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza kwa simu na mmoja wa maofisa wa Bandari ya Dar es Salaam baada ya kutembelea ofisini kwake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), Giliadi Ngewe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa pamoja na maofisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), wakishuhudia moja ya wakala wa meli akiwa amefunga ofisi kinyume cha maelekezo ya Serikali ya kufanya kazi saa 24.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...