
Wachezaji wa Simba SC, Nicolaus Gyan na Asante Kwasi wakiwasili leo jijini Dar es Salaam kutokea visiwani Zanzibar baada ya kuondolewa katika Michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi A.
Mshambuliaji wa Wekundu wa Msimbazi, Shiza Ramadhani Kichuya akizungumza na waandishi wa habari bandarini hapo mara baada ya kuwasili leo Jijini Dar es salaam akitokea visiwani Zanzibar. Simba imendolewa katika Michuano ya Kombe la Mapinduzi .
Baadhi ya washabiki wa Simba SC wakishangilia pindi timu hiyo iliporejea Dar baada ya kuondolewa katika Michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Mshabiki wa Simba SC, Willium Mazoba akizungumza na Michuzi Blog amesema kuwa amesikitishwa kwa timu yake kupoteza michuano hiyo na kuwataka walimu kujipanga kwa ajili ya ligi kuu Tanzania Bara. (Picha na Agness Francis wa Globu ya Jamii)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...