MAKAMU
wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuchana na vitendo
vya uharibifu wa mazingira kwa lengo la kujiepusha na athari zitokanazo
na mabadiliko ya tabia nchi.
Mama Samia
amesema hayo leo jijijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya
kutembelea miradi ya ujenzi wa kuta za kingo katika Bahari ya Hindi eneo
la Ocean Road na Kigamboni.
Amesema kuwa
Tanzania imeharibu mazingira yake kwa kiasi kikubwa hali inayofanya
sehemu kubwa ya maeneo yote kuwa na hali tofauti na tulivyotegemea.Ametoa
mfano Mji wa Dodoma ambao watu wamekata miti yote na hivyo kusababisha
eneo hilo kuwa jangwa kiasi cha kusababisha maafa pindi mvua
zinaponyesha.
Ametaja kuwa mikoa mingi ambayo
iliyokuwa na baridi sasa hivi imekuwa ikiongoza kwa joto sawasawa na
mikoa iliyopo Pwani kwa mfano mikoa ya Kilimanjaro kila ukiangalia
utabiri wa hali ya hewa unaambiwa ina nyuzi joto 32 hadi 33, kiasi
ambacho awali haikuwahi kufikia hapo. Amesema
adhabu yote hiyo na athari zinazoonekana sasa inatokana na uharibifu
huo mkubwa wa mazingira unaofanywa na baadhi ya wanachi kwenye maeneo
mbalimbali nchini .
“Napenda kutumia mfano
anaotumia Papa Francis kuwa ukimkosea mwanadamu utakwenda kulia kanisani
au Msikitini utasamehewa lakini ukiyakosea mazingira hayana Msikiti
wala Kanisa yatakuadhibu mpaka utakaporudi kuwa rafiki tena,"amesema
Makamu wa Rais .
Ameongeza kuwa "Nasi
tumeharibu mazingira kwa kukata miti, kuchimba mchanga katika fukwe na
matokeo yake bahari imepata nguvu ya kula ardhi yetu,hivyo turekebishe
tulipoharibu ili kurudisha urafiki huu".Amesema
kwa Mkoa wa Dar es Salaam wakazi wake wamekuwa wakitupa taka katika
mitaro na ikiziba inaleta madhara ya mafuriko, hivyo hiyo ni hasara kwa
Taifa kwa kuwa tunatumia muda mwingi kutoa pole na anayepewa pole
hutegemea uende na chochote umsaidie kama mahindi na fedha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...