Na Agness Francis, Globu ya Jamii
WAFANYABIASHARA
wa kuku katika soko la Kuku lililopo Shekilango jijini Dar es Salaam
wamesema kwa sasa soko limekuwa gumu kidogo kutokana na kupungua kwa
wateja tofauti na siku za nyuma.
Wakizungumza
na Michuzi Blog, leo sokoni hapo ,wafanyabishara hao wamesema hali hiyo
imewafanya wawe katika wakati mgumu kurudisha faida.
Mmoja
wa wafanyabishara wa kuku sokoni hapo Mussa Shaaban amesema changamoto
ya wateja wa kuku kupungua imekuwa kubwa na hivyo kijikuta wakiwa na
hali ngumu kiuchumi kwani kuku hao kabla ya kununuliwa wanahitaji
kuhudumiwa na hiyo nayo inahitaji gharama yake.
Pia
amesema changamoto nyingine kwenye biashara hiyo ni baadhi ya kuku
kufia njiani kutokana na umbali mrefu wanaotumia wakati wa kuwasafirisha
hadi kufika sokoni hapo kwani wanawanunua mikoani.
Kuhusu
bei, amesema wao wananunua kuku wa kienyeji kwa Sh 13,500 hadi Sh 14,
000 na kisha wao huuza kuku mmoja kwa Sh 18,000 hadi Sh.20,000. Pia
amesema kwa kuku wa kisasa wamekuwa wakiwauza kwa Sh 6,300.
Pia
imeelezwa na wafanyabishara hao kuku wa mayai wao wananunua kuku mmoja
kwa Sh 8,000 hadi Sh 8,500 na kisha wanawauza kwa reja reja kwa Sh10,000
na kwa jumla wanauza Sh 9000 hadi Sh.9500.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...