Na Neemalisa Nambeye, Globu ya Jamii
WAFANYABISHARA wa ndizi katika soko la Mahakama ya Ndizi lililopo Mabibo jijini Dar es Salaam wamesema kuwa katika soko hilo bei ya mkungu mmoja wa ndizi wanauza Sh.15000 ambayo iko chini zaidi ukilinganisha na masoko mengine.
Wakizungumza leo na Michuzi Blog sokoni hapo, baadhi ya wafanyabiashara ya ndizi wamesema wanauza bei hiyo kutokana na wingi wa ndizi zinazofika sokoni kwao lakini pia kule ambako wananunulia bei ya manunuzi iko chini.
Imefahamika wakati bei ya mkungu wa ndizi ikiwa Sh.15000 kwenye soko hilo masoko mengine likiwamo soko la Buguruni jijini Dar es Salaam baadhi ya wafanyabiasha wanauza mkungu mmoja wa ndizi kati ya Sh. 30,000 hadi Sh.35.000.
Wafanyabiashara hao wa soko la Mahakama ya Ndizi wameeleza kuwa idadi ya wanunuzi wa ndizi ni kubwa sokoni hapo lakini kikubwa ambacho wanajivunia ni wingi wa ndizi zilizopo.
"Bei yetu iko tofauti na maeneo mengine,hapa kwetu mkungu mmoja tunauza Sh.15000 lakini masoko mengine bei iko juu kidogo.Sababu kubwa tunakofuata ndizi tunanunua kwa bei yenye unafuu na hivyo nasi kurudisha unafuu huo wa bei kwa wateja wetu,"wamesema wafanyabiashara hao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...