Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi ameitaka Mahakama kutenda Haki bila kufungwa na masharti ya kiufundi yanayoweza kukwamisha Haki kutendeka.

Pia ameitaka kutoa fidia ipasayo, kukuza usuluhishi ipasavyo, kukuza usuluhishi baina ya watu husika katika migogoro  na watoe haki bila kujali sababu za hali ya mtu kijamii ama kiuchumi

Waziri Kabudi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifunga maonesho ya Wiki ya Sheria ambayo kilele chake kinatarajiwa kufanyika kesho katika Viwanja vya Mahakama vya Chimala jijini. Kauli mbiu katika siku ya sheria mwaka huu inasema, Matumizi ya Tehama katika utoaji haki kwa wakati na kuzingatia maadili.

Waziri Kabudi pia ameitaka Mahakama ipunguze kuchelewesha kesi bila sababu za msingi na iongeze kasi ya usikilizwaji wa Mashauri kwa 

Ameongeza Wizara inathamini maonesho ya siku ya sheria na maendeleo yanayofanywa na Mahakama katika kuendeleza kuboresha mfumo wa sheria na kwamba Mahakama imekuwa ya kwanza kubadilika katika sekta ya sheria. Hivyo Wizara itahakikisha maboresho ya mahakama yanafanikiwa.

Kabla ya ufungaji wa maonesho hayo, Waziri Kabudi pia amezindua  Mahakama ya Mwanzo na Mahakama ya Wilaya Kigamboni.

Akizindua jengo hilo la Mahakama lililogarimu zaidi ya Sh.milioni 500  Prof.Kabudi amesema, mkakati wa Mahakama hadi kufikia mwaka jana walikuwa wanahitaji  Mahakama Kuu 19, Mahakama za Hakimu  Mkazi 14, Mahakama za Wilaya 109, Mahakama za Mwanzo 3003 huku wakiwa na uhitaji mkubwa wa ukarabati wa mahakama nyingi nchini. 

Aliipongeza Mahakama kwa ubunifu, umakini na ufanisi waliouonesha kwa kufanya utafiti wa kutumia Moladi na ujenzi bora, imara na wenye gharama nafuu. Prof. Kabudi pia ameipongeza mahakama kwa kujenga majengo hayo katika wilaya mpya, hasa Kigamboni na amewataka kutafuta viwanja zaidi ili jitihada za kuongeza mahakama Kigamboni zifanyike kwa kuwa ipo moja tu.

Waziri wa katiba na Sheria, Profesa Pamalagamba Kabudi akizungumza na wananchi pamoja na watumishi wa Mahakama wakati wa uzinduzi mahakama ya mwanzo na Wilaya ya Kigamboni, kulia kwake ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania, Ferdnandi Wambari na kulia kwake ni Jaji Mkuu  Kuu Zanzibar Omary, Othaman Makungu.
 Waziri wa katiba na Sheria Profesa Pamalagamba Kabudi akipanda mti katika jengo jipya la mahakam ya mwanzo na Wilaya ya Kigamboni, baada ya kumaliza kuzindua mahakama hiyo mpya.
Waziri wa katiba na Sheria Profesa Pamalagamba Kabudi akiwa katika Picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa mahakama nchini Tanzania na Zanzibar

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...