Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii 

WAMETAFUTA mbinu mbadala! Ndivyo unavyoweza kuelezea kinachoendelea kwenye baadhi ya magereza yaliyopo nchini kwa baadhi ya wafungwa na mahabusu kutumia sehemu zao za siri kwa ajili ya kuingia na simu za mkononi pamoja na sigara.

Sheria za magereza kuna baadhi ya vitu vimepigwa marufuku ikiwamo simu ya mkononi, dawa za kulevya, visu ,nondo na sigara lakini baadhi ya mahabusu na wafungwa wamekuwa wakiingia nazo kwa kutumia mbinu mbalimbali.

Kwa mujibu wa Mrakibu Msaidizi wa Magereza, makao makuu kitengo cha sheria Absalom Mokily ameiamba Michuzi Blog kwenye mahojiano maalumu yaliyofanyika leo alipokuwa kwenye maonesho ya Wiki ya Sheria inayoendelea jijini Dar es Salaam kuwa kuna mbinu nyingi wanazozitumia mahabusu na wafungwa kuingia na vitu hivyo.

SEHEMU ZA SIRI ZINATUMIKAJE? IKO HIVI .

Akielezea zaidi kuhusu baadhi ya wafungwa na mahabusu kutumia sehemu zao za siri kuingia na vitu ambavyo vimepigwa marufuku , Mokiry amesema wenye tabia hiyo wamekuwa wakijaza mizigo kupitia njia  za haja kubwa na njia ya mkojo.

Amesema kuwa wanaoingia na vitu hivyo hata askari Magereza wanashindwa kubaini kutokana na utaalamu wanautumia kificha vitu hivyo vilivyopigwa marufuku kuingizwa magerezani."Unaweza kuwapekua na usione chochote, hivyo unapomruhusu aondoke, anachokifanya anakwenda chooni na kisha kutoa vitu alivyoficha kwenye  sehemu zake za siri,"ameeleza.

Mokily amesema kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Magereza namba 149 ya mwaka 2003 imezuia baadhi ya vitu kuingizwa magerezani.Ametaja baadhi ya vitu hivyo ni ni silaha, simu, visu, nondo, bangi, tumbaku na simu za mkononi."Ni marufuku kuingia na vitu,"amesema.

Amesema kuwa tabia hiyo si tu kwa baadhi ya wafungwa na mahabusu wa kiume tu bali hata wanawake nao wanatabia hiyo kwa kuchukua vitu hivyo na kuficha sehemu zao za siri."Wanawake wenye tabia ya kuficha vitu wanachokifanya ni kukimbilia chooni na kisha huvitoa na baada ya hapo utashangaa kuona wanawasiliana na watu walioko nje kwa kutumia simu ambazo wameingia nazo kwa mtindo huo,"amesema.

Mrakibu wa Magereza Kitengo cha Sheria, Absalom Mokiry akifafanua mambo mbali mbali juu ya wafungwa na mahabusu waliopo mahakamani ikiwemo kuingiza simu na vitu vilivyokatazwa gerezani kwa kutumia njia zisizostahili.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...