Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

WANAWAKE wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo kuombwa rushwa ya ngono wametakiwa kuripoti katika vyombo vya sheria ili kupatiwa msaada.

Akizungumza na Michuzi blogu, Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Ofisa Mradi wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), Asha Komba amesema rushwa ya ngono imekuwa jambo la kawaida katika jamii huku walengwa wanaofanyiwa vitendo hivyo wanashindwa  kutoa taarifa.

Komba amesema kitendo cha mwajiri au mwalimu kushawishi kufanya mapenzi kwa kuahidi kumpatia kazi au kufaulu masomo, inatambuliwa kama rushwa ya ngono.

Amesema, katika kukabiliana na hilo, wanatoa mafunzo kwa wanasheria, mahakimu, majaji na polisi kuhusu kumaliza unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo rushwa ya ngono kwani hupunguza ufanisi wa kazi na kurudisha maendeleo,Ameongeza wamekuwa wakikusanya kesi za unyanyasaji na kuzichapisha ili Majaji na Mahakimu waweze kuzitumia wakati wa kutoa maamuzi yao.

Kwa upande wake, Mwanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC), Ruth Ndagu amesema adhabu ya mtu yoyote anayeomba rushwa ya ngono hufukuzwa kazi kwa matumizi mabaya ya madaraka au kifungo cha kuanzia miaka mitatu hadi mitano au kulipa faini ya kuanzia Sh.milioni moja hadi Sh.milioni tano.

Ndagu alisema rushwa ya ngono inafanyika kwa usiri na ni watu wachache wanaotoa taarifa kuhusu matendo hayo.

"Tunatumia sheria  ya kujamiiana ya mwaka 1999 katika kumshtaki anayetuhumiwa kwa rushwa ya ngono ambayo inakataza kuhusu kumdhalilisha mtu hata kwa kumshika maungo yake au kufanya mapenzi kinyume na maumbile, pia tunatumia sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11, kifungu namba 25 ya mwaka 2007," amesema Ndagu.

Amesisitiza kuwa wamekuwa wakipokea zaidi matukio ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto ambapo kwa mwaka wanaweza kupokea matukio 20 hadi 30 na kwamba watu wazima hawatoi taarifa.
 Ofisa mradi wa chama cha majaji wanawake Tanzania, TAWJA, Asha Komba akizungumza na mmoja wa mwananchi aliyejitokeza katika viwanja vya Mnazi Mmoja kwenye maonyesho ya wiki ya sheria, kupata ushauri juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo rushwa ya ngono.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...