Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeshiriki katika Wiki ya Sheria kwa kutoa ushauri na kupokea malalamiko mbalimbali kutoka
kwa wananchi waliofika kutembelea mabanda hayo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Katika kuelekea maadhimisho ya wiki ya sheria kesho, maonesho hayo yaliyoanza Jumapili ambapo NHIF wameweza kutoa huduma ya
upimaji magonjwa yasiyoambukizwa sambamba na ushauri nasaha kwa wananchi mbalimbali.
Mtaalamu wa Kisukari kutoka Hospitali ya Amana Dk.Natalius Kapilima amesema wananchi wengi waliojitokeza kupata huduma ya vipimo wamekutwa wana uzito mkubwa unaotokana na ulaji usiofaa na kutokufanya mazoezi ya viungo vya mwili Magonjwa yaliyokuwa yanapimwa katika banda la NHIF ni kisukari, presha (BP), uwiano wa uzito na urefu wa mtu pamoja na maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU) na takribani wananchi 170 waliweza kupata huduma hiyo.
NHIF wameweza kuandikisha wanachama wapya wanaotaka kujiandikisha na mfuko huo wa bima hususani kwa TOTO afya Kadi kwa ajili ya watoto wadogo chini ya miaka 18.

Nesi Catherine Moshi akiwa anachukua kipimo cha damu kutoka kwa mwananchi aliyefika kwenye banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika maonyesho ya wiki ya Sheria nchini.
Afisa wa Sheria kutoka Makao Makuu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Tamasha Magongo akimuelekeza mwananchi aliyefika kwenye band lao alipoleta malalamiko yake.

Mfanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Victor Wanzagi akitoa maelezo kwa mwananchi aliyefika kwenye banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika maonyesho ya wiki ya Sheria nchini.
Mtaalamu wa Kisukari kutoka Hospitali ya Amana Dr Natalius Kapilima akimsikiliza mwamachi aliyefika kwenye banda la Mfuko wa Taifawa Bima ya Afya (NHIF) katika maonyesho ya wiki ya sheria nchini.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...