
Na Tiganya Vincent
JESHI la Polisi Mkoa wa Tabora linakabiliwa na uhaba wa nyumba za kuishi Askari wake jambo linalowafanya wengi kupanga uraini ambapo sio salama kulingana na shughuli zao.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) Wilbroad Mtafungwa wakati wa hafla fupi ya sifa na zawadi kwa askari Polisi vyeo mbalimbali mkoani humo waliotumia Jeshi hilo kwa weledi na nidhamu.
Alisema kuwa ambazo wanaishi Maaskari ni kongwe na chakavu ambapo zinahitaji ukarabati mkubwa na kujengwa mpya ambazo zitasaidia Askari waliopanga uraiani kuondoka huko na kuisha katika nyumba hizo.
SACP Mtafungwa alisema kuwa Askari wanaoishi kambini hivi sasa ni 327 na waliopo uraiani ni 853 na hivyo kufanya Askari wengi kuwa uraiani.Kufuatia hali Kamanda huyo wa Mkoa aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia Jeshi la Polisi ili liweze kupata makazi katika maeneo yao maalum ili waweze kufanyakazi kwa ufanisi wa hali ya juu zaidi.
Alisema kuwa kama wanavyochangia katika Ujenzi wa Vituo mbalimbali vya Polisi ni vema wakachangia pia ujenzi wa nyumba kwa ajili ya makazi ya Polisi ili kuondoa tatizo la ukosefu wa nyumba kwao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...