Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
TAASISI
ya Msichana Initiative imezindua kitabu kidogo kinachozungumzia haki
mbalimbali za watoto na kupinga ndoa za utotoni kwa mtoto wa kike.
Uzinduzi
wa kitabu hicho umefanyika leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa
tasisi hiyo Rebeca Gyumi amesema ni vema watanzania wakakitumia kitabu
hicho kilichoandaliwa na timu ya mawakili kwani kimeandikwa kwa lugha
rahisi zaidi kuhusu maamuzi yote yanayotolewa na Mahakama Kuu ya
Tanzania Julai 8 mwaka 2016.
“Mahakama Kuu,
kupitia Majaji wake katika kesi hii waliona kuwa vifungu hivi haviendani
na Katiba ya nchi.Pia vinabagua haki za watoto wa kike ukilinganisha na
haki za watoto wa kiume."Vifungu hivyo
vinaruhusu mtoto wa kiume kuoa katika umri wa miaka 18 na mtoto wa kike
kuoelewa katika umri wa miaka 14 na 15 kwa ruhusa ya Mahakama na
wazazi,"amesema Gyumi.
Amesema vifungu hivyo
vinachochea kwa kiasi kikubwa suala la ndoa za utotoni hasa kwa watoto
wa kike na kutaja Tanzania ni moja ya nchi yenye asilimia kubwa ya
tatizo la ndoa za utotoni ikilinganishwa na nchi zingine za ukanda wa
Afrika Mashariki ukiacha Uganda.Ameongeza
wasichana wawili kati ya watano huolewa kabla ya kufikia umri wa miaka
18 na wasichana hao hukumbwa na changamoto nyingi wanapoingia katika
ndoa.
"Wanaolewa wakiwa na mri mdogo wanapopata
mimba wakati wa kujifungua wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kupoteza
maisha kwa sababu via vyao vya uzazi bado ni vichanga.Pia huwanyima haki
yao ya kupata elimu,"amesema.
Gymi amesema
kupitia kitabu hiki chenye maamuzi ya Mahakama Kuu, jamii itaelewa na
kutambua zaidi namna ambavyo vifungu hivyo kandamizi kwa watoto wa kike
na kuona haki ambazo zimetambuliwa kisheria kupitia hukumu hiyo, pia
madhara ya ndoa za utotoni .
Amefafanua
Msichana Initiative pamoja na wadau wengine wanaamini suala la ndoa za
utotoni litakoma endapo jamii itakuwa tayari kuwashika mkono watoto wa
kike kwa kuwalinda na kutetea haki zao msingi.
Mkurugenzi wa Tasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akiwa katika picha ya pamoja wageni waalikwa wakiwa wameshika kitabu kidogo kinachozungumzia haki na mambo mbalimbali ya haki za watoto.
Mkurugenzi wa Tasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kitabu Kidogo kinachozungumzia haki na mambo mbalimbali y watoto na kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
Mkurugenzi wa Tasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akiwa katika picha ya Pamoja na wadau wakati wa uzinduzi wa Kitabu Kidogo kinachozungumzia haki mambo mbalimbali za watoto na kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...