Licha
ya Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Mbeya, Wananchi katika Kata na
vijiji mbalimbali mkoani humo, wameendelea kuhamasika kujitokeza kwa wingi
kusajili kupata Vitambulisho vya Taifa.
Katika
Kata ya Ilemi amkusanyiko wa wananchi umekuwa mkubwa; ikidhihirisha ni kwa
namna gani wananchi wamekuwa na uelewa mpana wa umuhimu wa Vitambulisho vya
Taifa; hususani katika kipindi hiki ambacho zoezi kwa sasa linaendelea.
Afisa
Usajili Wilaya ya Mbeya Bi. Alavuya Ntalima amesema katika Kata ya Ilemi zoezi
limeanza Jumatano tarehe 3/01/2018 na linahusisha Kata za Iganzo, Isanga,
Sisimba, Mabarini, Maendeleo pamoja na Forest.
Wakizungumzia
zoezi la Usajili linaloendelea katika Kata zao Watendaji wa Serikali za vijiji
wameahidi kuendelea kushrikiana kwa
karibu na Mamlaka kuhakikisha wananchi wote wanaoishi kwenye vijiji vyao na
wenye sifa wana sajiliwa na kupata Vitambulisho vya Taifa ndani ya muda uliopangwa.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti Wananchi wamepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali
kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) hususani hili la kuwatambua
wananchi na kuwapatia Vitambulisho vya Taifa ambavyo vitawapa fursa ya kufanya mambo
mengi na kutambulika katika shughuli mbalimbali za kijamii.
Afisa
Usajili Mamlaka ya Vitambulsho vya Taifa Ndugu Lodrick Hawonga, akiwapatia
wananchi wa Kata ya Ilemi huduma ya Usajili kwa kuwajazia fomu za maombi ya
Vitambulisho vya Taifa.
Baadhi
ya Wananchi wa Vijiji mbalimbali kata ya Ilemi wakikamilisha usajili wa awali
kwa kujaza fomu za maombi kwa wale ambao hawakuwa wamekamilisha zoezi hilo,
kushoto ni Mjumbe wa kata hiyo Ndugu Martini Mpwani akiwasaidia kujaza barua za
Utambulisho kwa wale waliokosa Viambatisho.
Mtendaji
wa kata ya Ilemi Ndugu Amiri Kassimu, akiwahakiki na kuwatambulisha Wananchi
wake kwa kuwagongea Muhuri wa Serikali ya Mtaa ya Ilemi pamoja na kuwaandikia
barua za utambulisho zitakazowawezesha kukamilisha hatua muhimu katika zoezi la
usajili Vitambulisho vya Taifa ambalo linahusisha uchukuaji alama za
Vidole, Picha na saini ya Kielktroniki
Wananchi
wakiwa wamepanga foleni nje ya moja ya Kituo cha Usajili wakisuburi kupatiwa
huduma hiyo licha ya Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali
Mkoani Mbeya.
Mmoja
wa Wananchi waliojitokeza kupatiwa huduma ya Usajili katika kituo cha Usajili
cha Mwamfute kata ya Ilemi akichukuliwa alama za Vidole katika zoezi la Usajili
lililohusisha uchukuaji wa alama za kibailogia, saini ya Kielektroniki pamoja
na Picha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...