
Naibu Waziri wa Maji na Umwangiliaji, Mheshimiwa Jumaa Aweso ameahidi serikali kupitia wizara ya Maji kulipa kwa wakati wakandarasi waaminifu wanaosimamia miradi ya Maji ili upatikanaji wa Maji uwe endelevu.
Aweso ameyasema hayo Jijini Dar kwenye siku yake ya nne ya kikazi alipokuwa akikagua maendeleo ya miradi ya Maji inayotekelezwa na Manispaa pamoja na Miradi ya DAWASCO na DAWASA.
"Wizara ya Maji inajitahidi kutengeneza miradi ya maji itakayomaliza tatizo la Maji kwa wananchi hususani wananchi wenye kipato cha chini hasa vijijini, hivyo mkandarasi atakayefanya kazi yake vizuri na kwa wakati sisi kama serikali hatutasita kumlipa kazi yake kwa wakati"alisema Aweso Katika ziara yake hiyo, Mheshimiwa Aweso alitembela miradi ya Maji ya Hondogo, Kibamba, Kingazi A pamoja na Mburahati.

Naibu Waziri wa Maji na Umwangiliaji, Mheshimiwa Jumaa Aweso akiangalia bomba lililopasuka.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Usambazaji Maji wa DAWASCO, Aaron Joseph juu ya tenki la maji la Kibamba na nyuma yao ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiko.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa tenki la Mradi wa Maji wa King’azi A, Kata ya Kwembe, Kibamba.
Mhandisi wa Mradi wa BORDA, Modekai Sanga ambao ndio wafadhili wa mradi wa kuchakata maji wa DEWAT uliopo Mburahati, akitoa maelezo ya mradi huo kwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...