Serikali ya watu wa Japan imekabidhi mradi wa Soko la Samaki la kimataifa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chato wenye thamani ya shilingi milioni 320 na kusaini makubaliano ya ukarabati wa barabara ya Mganza - Kasenda ili kurahisisha usafirishaji wa mazao ya ziwani.
Akizungumza baada ya kukabidhi mradi huo kwa Serikali Balozi wa Japan nchini Tanzania Mheshimiwa Yoshida Masaharu amesema mradi huo umetolewa na Serikali ya Japan kwa watu wa Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa urafiki wa siku nyingi katika utekelezaji wa miradi ya kilimo na uvuvi. ''Mradi wa huu ulitolewa baada ya kuona soko la Kasenda liko katika hali mbaya na samaki kuharibika kwa kukosa miundombinu ya kuhifadhi ndipo Japan ikachukua hatua za haraka kwa kutoa fedha dola za kimarekani 148,146 kwa ajili ya kujenga soko na kukarabati soko la zamani''. Utekelezaji wa mradi ulianza mwaka 2017 na sasa wananchi wanaendelea kunufaika.
Awali akisoma taarifa ya mradi huo kabla ya makabidhiano mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato Joel Hari amesema mradi unahusisha ujenzi wa ghala kubwa la kuhifadhia samaki na ukarabati wa sokola zamani.Ameeleza kuwa soko lipo chini ya Halmashauri ya Chato likiwa na wanachama 241 huku likikasimiwa kukusanya shilingi milioni 140 kwa mwaka huku likitoa huduma kwa nchi za Rwanda,Burundi, Uganda na Congo DRC.haa za kutoka ziwani.

Balozi
wa Japan Nchini Tanzania. Yoshida Masaharu pamoja na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Chato, bw Joel Hari wakiweka jiwe la
makabidhiano ya mradi wa Soko la Kimataifa la Samaki ambalo
limefadhiliwa na Serikali ya Japan kwa Gharama ya Shilingi milioni 320
kijiji cha Kasenda Chato.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel(kushoto) na Balozi wa Japan
Nchini Tanzania, Yoshida Masaharu wakisaini kitabu cha wageni baada ya
kuwasili kijiji cha Kasenda kwa ajili ya Makabidhiano ya Mradi wa Soko
la Samaki la Kimataifa na kusaini mkataba wa ukarabati wa barabara yenye
urefu wa Kilometa 1 ya kutoka Mganza kwenda Kasenda.
Balozi
wa Japan Nchini Tanzania Mheshimiwa Yoshida Masaharu na Viongozi wa
Mkoa wa Geita na Wilaya ya Chato baada ya makabidhiano ya mradi wa
ujenzi wa Soko la Samaki la Kimataifa la Kasenda Wilayani Chato.Watatu
kutoka kushoto kwa balozi ni Waziri wa Nishati (Mb) Mheshimiwa Medard
Kalemani na Shaban Ntarambe Mkuu wa Wilaya ya Chato na Kulia kwa balozi
aliyevaa miwani na suti ya kijivu ni Mkuu wa Mkoa wa Geita mhandisi
Robert Gabriel pamoja na Bw; Joel Hari Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Chato.
Mradi
wa ujenzi wa Soko la kimataifa la Samaki la Kijiji cha Kasenda Wilayani
Chato uliojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan na kukabidhiwa kwa
Halmashauri ya Wilaya ya Chato.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...